Connect with us

Top Story

TUZO ZA UEFA ZAUNGANISHWA NA BALLON D’OR.

Tuzo za UEFA kuanzia sasa hazitakuwepo baada ya kuunganishwa pamoja na za Ballon d’Or.

Shirikisho la soka Barani Ulaya [ UEFA ] limefikia makubaliano na Group Amaury [wamiliki wa vyombo vya habari vya France Football na L’Equipe ] ili kuboresha hadhi ya tuzo za Ballon d’Or duniani

Muunganiko huo ni ishara ya kumalizika kwa tuzo za UEFA zinazotolewa mwezi Agosti kila mwaka, isipokuwa tuzo ya Rais ambayo bado itatolewa pamoja na droo za Ligi ya mabingwa

Chini ya ushirikiano huo mpya, UEFA imesema tuzo zote za Ballon d’Or zitasalia pamoja na kuongezwa kwa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa wanaume na wanawake.

Groupe Amaury inaendelea kuwa na haki juu ya chapa ya Ballon d’Or na mfumo wa upigaji kura hautabadilika kazi ya UEFA itakuwa ni kuzitangaza kibiashara na kuandaa event hiyo kila mwaka.

Makala Nyingine

More in Top Story