Connect with us

Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania

TANZANITE KUIKABILI NIGERIA LEO CHAMAZI.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite, leo ina kibarua kizito cha kuikabili timu ya Taifa ya Nigeria katika mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia, mchezo huo utachezwa kuanzia saa 9:00 Alasiri katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar Es Salaam.

Mchezo huo hautakuwa na kiingilio, tayari nyota kadhaa wamesha jiunga na kikosi hicho na kinachosubiriwa ni muda ufike. Kocha mkuu wa kikosi cha Tanzanite Bakari Shime amesema hadi kufikia hii leo maandalizi yapo vizuri.

Hadi hivi sasa maandalizi yapo vizuri, vijana wataenda kupambana, panapo majaaliwa tutaibuka na ushindi hii leo. Ni mechi yetu ya kwanza lazima tuweke msingi kuelekea katika mchezo wa marejeano nchini Nigeria.

Tupo nyumbani, kwa vyovyote vile lazima tushambulie kwasababu lazima tupate magoli ya kutosha lakini lazima pia tujilinde vizuri ili kuwazuia wapinzani wetu wasipate goli la mtaji.

Bakari Shime, kocha mkuu wa kikosi cha Tanzanite.

Nahodha wa kikosi cha Tanzanite Noela Luhala amewaomba mashabiki kujitokeza katika mchezo wa leo ili kuwapa nguvu na ari ya kupambana ili wapate ushindi.

Wachezaji tumejiandaa vizuri na tunapokea vizuri maelekezo ya mwalimu wetu kwaajili ya mchezo wetu dhidi ya Nigeria.

Nigeria tunawafahamu, tulikuwa nao kwenye mashindano ya kombe la Dunia chini ya miaka 17 huko India, hivyo tunaamini mchezo utakuwa wa ushindani.

Tunawaomba mashabiki na Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kwaajili ya kutushangilia na kutupa sapoti katika mchezo huu, tunaamini tutashinda hatutawaangusha.

Noela Luhala, Nahodha wa kikosi cha Tanzanite, akizungumza kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Nigeria.

Makala Nyingine

More in Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania