Connect with us

NBA

DRAYMOND GREEN YAMMKUTA MAZITO NBA

Mchezaji wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Golden State Warriors inayoshiriki ligi ya kikapu nchini Marekani, NBA, Draymond Green amekumbana na rungu la kifungo cha mechi 5 kuanzia mchezo dhidi ya Oklahoma City Thunder jana sambamba na faini ya kukatwa mshahara wa takribani $ 769,704 za kimarekani  sawa na takribani Bilioni 1.2 za Kitanzania kutokana na kosa lake la kummkaba mchezaji wa Minnesota Timberwolves, Rudy Gobert.

Draymond alifanya tukio hilo wakati akiingilia ugomvi kati ya mchezaji mwenzake Klay Thomson na Jaden McDaniels wa Timberwolves, ambapo muda huo Rudy Gobert alikuwa akijaribu kuwaamulia ndipo Green alikuja na kummkaba koo kwa nyuma.

Kitendo hicho kilienda sambamba na wachezaji Klay Thomson, Jadon McDaniels na Draymond Green kuondolewa kwenye mchezo papo hapo kwenye mchezo ulioisha kwa Timberwolves kuwanyuka Warriors 104-101.

Makamu wa Raisi Mtendaji ambaye pia ni Mkuu wa Uendeshaji wa mpira wa kikapu NBA, Joe Durmas alisema kuwa adhabu hiyo kwa Green ni kutokana na historia na rekodi zake mbaya za nyuma za matukio yanayofanana na hayo ya michezo isiyokuwa ya kiungwana kwenye michezo.

Katika hatua nyingine, Thomson, McDaniels na Gobert wote wapigwa faini ya $25,000 za kimarekani sawa na Milioni 63 za Kitanzania.

Makala Nyingine

More in NBA