Connect with us

CAF Champions League

AL AHLY KUKIPIGA LEO KABLA YA KUIKABILI YANGA.

Klabu ya Pyramids anayoitumikia mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Young Africans Fiston Kalala Mayele itashuka dimbani hii leo majira ya saa kumi na moja [17:00] jioni kuikabili Ismaily SC.

Baada ya mchezo huo klabu ya Pyramids itasafiri hadi nchini Mauritania kwaajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wa hatua ya makundi dhidi ya FC Nouadhibou utakaopigwa December 2 majira ya saa moja jioni [19:00].

Pyramids ipo kundi A pamoja na klabu za Mamelodi Sundowns, TP Mazembe na FC Nouadhibou baada ya mchezo huu pia itakuwa na mchezo wa Ligi nchini Misri December 6 dhidi ya El Gounah.

Klabu nyingine itakayoshuka dimbani hii leo ni Al Ahly ambayo inacheza mchezo wake wa Ligi kuu nchini Misri majira ya saa mbili usiku dhidi ya Smouha SC kabla ya kuianza safari ya kuja nchini.

Al Ahly ina kibarua kizito mbele ya Young Africans SC December 2, kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika. Baada ya mchezo huo itarejea nyumbani kucheza mchezo wake wa Ligi dhidi ya ZED FC, December 6 saa 17:00.

Young Africans haijacheza mchezo wowote tangu mara ya mwisho ipoteze 3-0 dhidi ya CR Belouizdad na inasubiri mchezo wa December 2 dhidi ya Al Ahly na kisha itacheza tena dhidi ya Medeama ugenini December 8 mwaka huu.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League