Connect with us

CECAFA

TANZANIA BARA U17 YATAKATA CECAFA.

Mashindano ya CECAFA U17 yanaendelea nchini Kenya, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakilishwa na timu mbili ambazo ni Zanzibar na Tanzania Bara.

Michuano hiyo inajumuisha timu nane [8] kutoka mataifa saba [7] yaliyopo ndani ya ukanda wa CECAFA, Mataifa hayo ni Kenya, Somalia, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania pamoja na Uganda.

Timu zote nane [8] zilipangwa kwenye makundi mawili [Kundi A na Kundi B] na timu mbili zitakazo maliza kinara kwenye kila kundi zitasonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano hii.

Kutoka Kundi A limeundwa na timu ya Taifa ya Kenya, Somalia, Rwanda na Sudan huku Kundi B likiundwa na Sudan Kusini, Tanzania, Zanzibar na Uganda.

Kundi B ndilo kundi lililohesabika kuwa gumu zaidi kitu ambacho kilizilazimsha timu kusubiri michezo yake ya mwisho ili kujua ni timu ipi itaenda hatua ya nusu fainali.

Jana kundi hilo lilifika tamati kwa michezo miwili kupigwa,

Tanzania Bara ilikuwa ikicheza dhidi ya ndugu zao Zanzibar na matokeo yakawa 1-1 katika uwanja wa Kakamega.

Timu zote mbili, Tanzania na Zanzibar zimemaliza michezo kwenye kundi zikiwa na alama sawa [4] na idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Hata hivyo Tanzania imesonga mbele kwenye michuano hii kwa kanuni ya FAIR PLAY kutokana na kuwa na kadi chache za njano [4] kuliko Zanzibar [5].

Uganda ilifuzu kwenye kundi hili baada ya kupata ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Sudan Kusini [2-0] na hivyo kiwafanya wafikishe alama sita [6] na kuwa vinara wa kundi hilo.

Nusu fainali Tanzania itakutana na timu ya Taifa ya Kenya U17 iliyomaliza kinara kundi A, siku ya December 5 huku mshindi wa tatu na fainali zinategemewa kupigwa December 8.

NUSU FAINALI

December 5.

12:00 Ugand vs Rwanda

Uwanja: Jomo Kenyatta

15:00 Kenya vs Tanzania

Uwanja: Jomo Kenyatta.

Makala Nyingine

More in CECAFA