Connect with us

Makala Nyingine

MTANZANIA AENDELEA KUAMINIWA SUPERSPORT UNITED

Mchezaji wa soka raia wa Tanzania, Abdulrazack Hamza anayekipiga kunako klabu ya Supersport United ya nchini Afrika ya Kusini ameendelea kuaminiwa na Mwalimi Gavin Hunt kuanza kwenye kikosi hicho.

Hamza alianza leo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya USMA ya Algeria kwenye uwanja wao wa nyumbani wakiambulia kipigo cha maba 2-0 kutoka kwa wageni wao. Kocha Hunt alisema machache kuhusu Hamza baada ya mchezo kumalizika.

Hakuna shaka juu ya uwezo wa Hamza. Ana umri mdogo bado na ana mengi ya kujifunza lakini mpaka hivi sasa ameshaonyesha uwezo wake kwenye michezo migumu kabisa tuliyocheza mfululizo. Kwa hivyo ndio ntaendelea kummpa nafasi kwakuwa licha ya kuwa mdogo ndio namna pekee ya kuwakomaza

Huu umekuwa ni mchezo wa tatu mfululizo Abdulrazack Hamza anaanza kwenye kikosi hicho itakumbukwa alianza dhidi ya Future ya nchini Misri wakifungwa 1-0 kwenye michuano ya CAF Kombe la Shirikisho lakini alicheza pia dakika 83 dhidi ya mabingwa watetezi wa PSL Mamelodi Sundowns wakifungwa tena kwa mabao 2-0.

Tunaendelea kummtakia Kheri mchezaji huyu wa zamani wa Namungo anayepeperusha vema bendera yetu ya Tanzania huko “Bondeni”.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine