Connect with us

AFCON

MRISHO NGASA KUUNGANA NA STARS AFCON 2023.

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limempa mwaliko mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Mrisho Khalfan Ngasa wa kushuhudia michezo ya fainali za mataifa ya Afrika zinazofanyika nchini Ivory Coast.

Mrisho Ngasa ni mchezaji pekee wa zamani kutoka Tanzania aliyepokea mwaliko rasmi kutoka shirikisho la soka Afrika.

Aidha Ngasa amelishukuru shirikisho la soka Afrika CAF na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kwa imani yao kwake.

“Nimefurahi kupokea Mwaliko Maalumu Kutoka Shirikisho la mpira wa miguu Africa CAF, nikiwa Mchezaji pekee wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kushiriki Michuano ya Mataifa ya Africa AFCON 2023, inayofanyika huko Ivory Coast”.

“Nachukua nafasi hii kulishukuru shirikisho la soka Afrika CAF kwa kuona umuhimu wangu na kuthamini soka la Tanzania, hii imekuwa faraja kwa wapenda Soka wote nchini Tanzania “.

“Naenda Ivory Coast kuiwakilisha Nchi yangu na Rais wangu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi mema aliyonayo kwenye michezo hususani mpira wa miguu”.

“Pia nishukuru viongozi wote kwa mchango wao wa mawazo ikiwemo shirikisho la soka la Tanzania TFF chini ya Rais wake Wallace Karia”.

“Tukutane Ivory Coast kuishangilia Taifa Stars”, amesema Mrisho Ngasa.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa mchezaji wa zamani kutoka Tanzania kupata mwaliko maalumu wa kushuhudia fainali za mataifa ya Afrika “AFCON” nchini Ivory Coast.

Kwenye michuano hii pia Taifa Stars itashiriki kwa mara ya tatu [Makala ya tatu] tangu michuano hii ianzishwe.

Makala Nyingine

More in AFCON