Connect with us

Makala Nyingine

BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MICHEZO NCHINI.

Salaam ziwafikie ndugu zangu viongozi wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Elimu nchini kwetu Tanzania.

Mimi kijana wenu napenda sana kuona vijana wakijikwamua kiuchumi kupitia mpira/soka lakini kwa wakati huo huo wakilisaidia Taifa kulitangaza kwenye ramani za soka Duniani.

Nisiwe na maneno mengi, barua hii inalenga hasa namna ya kulifanya Taifa letu lipige hatua kwenye soka na inawezekana ikawa hivyo, Mheshimiwa Rais anapenda sana soka na hakuna kinachoshindikana.

Tanzania ina zaidi ya watu Million 60, katika hao kuna vijana wengi wenye vipaji vikubwa waliamua kustaafu kucheza mpira wakiwa wadogo kwasababu hakuna mwendelezo wanaouona, kwasasa wana lia hawana ajira.

Ili kupunguza tatizo la Ajira nchini, tunaweza kuwekeza zaidi katika soka, kupitia mashindano ya Umisseta na Umitashumita yanayoendelea kuchezwa kwenye kila mkoa na kila Wilaya na hatimae kitaifa.

Mashindano hayo kwasasa hayana nguvu na bado yana changamoto kubwa kutokana na mfumo wa ukusanyaji wa vipaji ulivyo na hii ni Tanzania nzima, kuna wachezaji nyota wanaachwa pengine kwasababu hawana chochote au hawana wa kuwasemea.

Sasa nini tukifanye ili kuboresha haya mashindano na mwisho wa siku tufaidike nayo kama Taifa ?

  1. Tunapaswa kutafuta mashirikiano na nchi zilizoendelea kisoka, kama Ubelgiji na Uholanzi.

Ushirikiano huu ulenge zaidi kwenye Academy zao, ambapo kama Taifa walau kila mwaka wachezaji watano au sita wanaofanya vizuri kwenye mashindano ya UMITASHUMITA na UMISSETA au mashindano ya Chuo waweze kwenda huko wakanolewe.

Na hao wachezaji watapatikana baada ya Scouts wa Academy hiyo kuwachagua wenyewe maana wao ndio wanajua watoto wa kuwafundisha mwisho wanapata kitu bora.

Faida yake.

  • Wazazi watawahimiza zaidi watoto wao wakasome kila pande ya Tanzania na wacheze mpira kwani watayaona manufaa kupitia vipaji vyao.
  • Tutatengeneza timu bora ya baadae kupitia nyota watakaopelekwa huko kila mwaka na huenda likatusaidia hili.
  • Tutapunguza tatizo la ajira kwa sehemu fulani, kwani hata watakaosalia kila mwaka wanaweza kucheza kwenye klabu zetu za ndani na wakalipwa pesa itakayo wakwamua wao.
  1. Tunapaswa kubadili muundo wa hayo mashindano UMISSETA na UMITASHUMITA.
  • Kwasasa mashindano hayo yanachezwa kwa mtindo wa mkoa kitaifa kwa maana kila mkoa unatengeneza timu moja baada ya kufanya mchujo wa wachezaji kitu ambacho sio kibaya lakini hakijatupa faida yoyote ile hivyo tunapaswa kubadili hii aina ya uchezaji.
  • Mfumo mzuri ni wa kutafuta Bingwa wa mkoa kwa maana kila shule ijitegemee, icheze iwe bingwa wa Wilaya kwa kuzifunga shule zingine na mwisho awe bingwa wa Mkoa na kisha akashiriki michuano ya kitaifa yeye mwenyewe.
    • Hapa baada ya kuwa bingwa wa Wilaya anaweza kusajili wachezaji wa shule zingine aliowaona ni bora kisha akaenda kuwatumia kwenye mashindano ya Mkoa, akiwa Bingwa pia awe na nafasi ya kusajili nyota wengine aliowaona wazuri kwenye timu zingine. • Baadae aende akacheze ngazi ya Taifa, ikiwa ni jina la shule yake.

Faida zake.

  • Shule zitajitangaza, wanafunzi watahudhulia shuleni, tutapunguza kuchagua wachezaji wa kufahamiana kama ilivyo sasa hivi na tutaibua vipaji kutoka kila pande ya nchi na hii pia itaongeza hamasa ya soka kwa vijana.
  1. Kuwa na Fainali ya UMISSETA na UMITASHUMITA kitaifa kwa shule ambazo zimefanikiwa kufika na zawadi ikiwa kubwa [Mfano: Bingwa anapata Million 100].

Itaendelea….

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine