Connect with us

Michezo Mingine

TANZANIA YAFANYA KWELI FUTSAL NAMIBIA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa FUTSAL imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Namibia kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu kucheza 2024 FUTSAL AFCON uliopigwa huko Windhoek, Namibia.

Nahodha wa Timu hiyo, mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na Mbeya City, Awadh Salum aliiongoza vema timu yake kupata ushindi huo muhimu ugenini ikiwa ndio mara ya kwanza Tanzania kushiriki mchujo huu wa michuano hii inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili mwaka huu.

Tanzania walikuwa kwenye uongozi tangu dakika 20 za kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 3-0 huku kipindi cha pili waliendelea kutawala matokeo wakipata bao la 4 mpaka dakika ya 30 licha ya Namibia kupata mabao hayo mawili, Tanzania waliongeza lingine 1 na kupata matokeo hayo ya 5-2.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika hapa Nyumbani, Dar es Salaam kati ya tarehe 9-11 mwezi Februari huku mshinda wa Jumla anatarajiwa kukata tiketi ya kushiriki AFCON itayofanyika Aprili, 2024 huko nchini Morocco. Morocco wanakuwa wenyeji wa michuano hii kwa mara ya pili mfululizo huku wakiwa ndio Mabingwa watetezi walipotwa mwaka 2020.

Timu za Morocco, Egypt na Angola wanatarajiwa kuungana na timu 5 zitakazofuzu hatua hii ya kufuzu ili kutimiza timu 8 zitakazopepetana huko Morocco ili kupata timu 3 zitakazoenda kuwakilisha CAF kwenye FUTSAL WORLD CUP itakayofanyika huko UZBEKISTAN baadae mwaka huu wa 2024.

Makala Nyingine

More in Michezo Mingine