Connect with us

CAF Champions League

ASEC: TUTAIFUNGA SIMBA TUANDIKE HISTORIA.

Klabu ya Asec Mimosas ina mpango wa kuandika historia mpya kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwa kumaliza vinara wa kundi B.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Asec Mimosas zinasema klabu hiyo imeandaa dozi maalumu kwaajili ya klabu ya Simba kwani wanazihitaji alama tatu kwaajili ya kuiandika historia hiyo.

Tunahitaji kuandika historia ya ushindi, imekuwa muda mrefu sasa hatujamaliza vinara kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, naamini safari hii tutamaliza vinara na tunatakiwa kuifunga Simba.

Tumefanya mazoezi maalumu kwa washambuliaji kwaajili ya kufunga tu maana hatuwezi kupata alama tatu bila kufunga, tutawafundisha soka Simba, zaidi ya mchezo wa kwanza.

alisema kiongozi ambaye jina lake hakutaka liwekwe wazi.

Klabu ya Simba inahitaji alama tatu muhimu pia ili iweze kujiweka kwenye mazingira rafiki ya kufuzu hatua ya robo fainali huku ikiwa imesalia na michezo miwili pekee.

Simba tayari ipo nchini Ivory Coast kwaajili ya mchezo huo wa pili baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Asec Mimosas.

Baada ya mchezo huu Simba itamaliza michezo yake ya hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Asec Mimosas tayari imefuzu hatua ya robo fainali rekodi pekee ambayo inaisaka ni kumaliza vinara wa kundi B, kundi hilo lina timu za Asec Mimosas, Jwaneng Galaxy, Simba na Wydad AC.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League