Connect with us

Makala Nyingine

YANGA KUANZA SAFARI YA MISRI LEO.

Klabu ya Yanga inatarajiwa kuanza safari hii leo majira ya saa 11:55 Jioni kuelekea nchini Misri kwaajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe ameeleza kuwa klabu hiyo inatarajiwa kusafiri na wachezaji 24, viongozi wa benchi la ufundi 13 na watendaji na maofisa 23.

“Timu inatarajia kuondoka saa 11:55 jioni kuelekea Misri, kuwasili Cairo ni saa saba usiku kuamkia kesho”.

“Tutaondoka na msafara wa watu 60, msafara huu umegawanyika makundi matatu, wachezaji 24, benchi la ufundi 13, na Watendaji/maofisa wakuu wa klabu 23”.

  • Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC.

Aidha kwa upande mwingine Afisa Habari Ali Kamwe amewapongeza wachezaji kwa kujituma kwao na kupata matokeo chanya kwenye mchezo dhidi ya CR Belouizdad [4-0] yaliyoiwezesha klabu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika.

“Niwapongeze wachezaji kwa kupambana na jitihada zao zikaenda kuzalisha furaha kwa mashabiki”.

“Jasho lao limekwenda kutengeneza rekodi kuwa klabu ya kwanza kushinda goli 4 dhidi ya timu kutoka ukanda wa kaskazini hususani taifa la kiarabu tena bingwa wa ligi.”

“Nitakuwa mkosefu wa fadhila kwa kushindwa kuwashukuru benchi letu la ufundi chini ya Miguel Gamondi, wameandaa wachezaji vizuri, kiakili na kimwili”.

“Unaongelea Belouzidad ambaye amecheza dakika 180 bila kuruhusu goli, na kufanikiwa kuwauzia Al Ahly kushindwa kulenganhata shuti moja”.

“Kimsingi kama wachezaji wasingeandaliwa vizuri basi isingekuwa shughuli nyepesi”.

Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Ijumaa hii saa moja [19:00] jioni kukamilisha michezo ya hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly nchini Misri na timu zote mbili zimefuzu, mshindi wa mchezo huyo atakuwa kinara wa kundi D.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine