Connect with us

Azam FC

YANGA NA AZAM VITA KUBWA LEO.

Young Africans imeshinda mara nyingi zaidi ya Azam katika michezo 20 iliyopita.

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajia kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam. Mchezo huo utazihusisha timu mbili kubwa za Jiji la Dar Es Salaam Young Africans na Azam.

Mchezo huu umetawaliwa na hisia kubwa kwa pande zote mbili, huku kila timu ikisema wataingia kwa tahadhari kutokana na ubora wa kila timu ulivyo msimu huu.

Azam FC ipo nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa na alama kumi na tatu (13) nyuma ya kinara klabu ya Simba yenye alama kumi na tano (15). Iwapo Azam itashinda leo itakwea kileleni mwa msimamo kwa kufikisha alama kumi na sita (16), Azam hadi hivi sasa haijapoteza mcheo wowote katika michezo mitano (5) iliyocheza, ikishinda michezo minne (4) na sare moja (1). Azam ina tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga nane (8).

Young Africans ipo nafasi ya Tatu ya msimamo ikiwa na alama 12, ikishinda michezo minne (4) na kupoteza mchezo mmoja (1), iwapo itashinda hii leo itakwea kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa kufikisha alama kumi na tano (15) iatakuwa na faida ya magoli mengi tofauti na Simba licha ya kulingana alama. Hadi hivi sasa safu ya ushambuliaji ya klabu ya Young Africans inaonekana kuwa bora zaidi ikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kumi na tatu (13).

Young Africans na Azam fc zimekutana mara 20 kwenye michuano yote toka mwaka 2015, katika michezo hiyo Young Africans imeshinda michezo tisa (9), Azam fc imeshinda michezo mitano (5), na zimetoka sare sita (6).

Magoli mengi zaidi kwenye mchezo mmoja ambayo Young Africans iliwahi kuifunga Azam fc ni goli 2-3 msimu uliopita wa 2022/23, Azam ikiwa nyumbani.

Kipigo kizito ambacho Azam iliwahi kuishushia Youn Africans ni cha goli 3-0 msimu wa 2018/19, Young Africans ikiwa nyumbani.

Mchezo wa mwisho wa timu hizi kukutana ni wa michuano ya ngao ya jamii iliyopigwa Jijini Tanga katika dimba la mkwakwani na Young Africans ikaibuka na ushindi wa goli 2-0.

Mara nyingi mchezo Kama huu unaamuliwa na ubora wa eneo la katikati mwa uwanja (Khalid Aucho, Mudathiri Yahya, Aziz Ki au Zouzoua Pacome) upande wa Azam (Feisal Salum, Sospeter Bajana na James Akaminko) ni vita ya mpira wa miguu kwenye eneo la kiungo .

Timu zote zina safu bora ya ushambuliaji upande wa Young Africans (Maxi Nzengeli, Clement Mzize na Kennedy Musonda), Upande wa Azam ( Price Dube, Idriss Mbombo na Abdul Sopu au Ayoub Lyanga) zinapokutana timu hizi kunakuwa na ushindani mkubwa sana.

Makala Nyingine

More in Azam FC