Connect with us

African Football League

ENYIMBA YATIA DOSARI AFRICAN FOOTBALL LEAGUE.

Mchezaji wa klabu ya Enyimba aliingia uwanjani akiwa amevaa jezi iliyoandikwa kwa mkono Jina lake na namba yake mgongoni.

Jana Ligi ya African Football League imeendelea kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti Barani Africa. Katika mchezo wa mapema TP Mazembe (DRC) ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi Esperance de Tunis.

Mchezo wa pili ulikuwa kati ya mwenyeji klabu ya Enyimba dhidi ya Wydad Casablanca, mchezo ambao ulimalizika kwa Wydad AC kuibuka na ushindi wa goli 0-1. Katika mchezo huo gumzo lilikuwa ni mchezaji wa klabu ya Enyimba Innocent ambaye aliingia uwanjani akiwa amevaa jezi iliyoandikwa kwa mkono jina na namba yake uwanjani.

Maoni ya wengi yanatafsiri kuwa ni fedheha na aibu kubwa kwa Ligi hii kubwa Barani Afrika na inayolenga kuziongezea thamani klabu mbalimbali zinazoshiriki mashindano haya. Timu shiriki kwenye mashindano haya zote nane (8) zinapokea kiasi cha $ 1 Million ambayo ni sawa na Billion 2.5.

Wakati wa ufunguzi wa mashindano haya Jijini Dar Es Salaam, Rais wa shirikisho la soka Barani Africa Patrice Motsepe alisema lengo la Mashindano haya ni klabu zipate pesa za kujiendeshea zenyewe na pia kuboresha miundo mbinu ya kilaklabu Barani Africa.

Makala Nyingine

More in African Football League