Connect with us

International Football

KOCHA WA ZAMANI SIMBA KUTANGAZWA BOTSWANA.

Shirikisho la soka nchini Botswana linatarajia kumtangaza hivi karibuni kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa hilo.

Shirikisho la soka nchini Botswana limefikia makubaliano na aliyewahi kuwa kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Mfaransa Didier Gomez Da Rosa ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Botswana. Shirikisho hilo lina mpango wa kumtambulisha hivi karibuni kuelekea michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.

Didier Gomez alifanikiwa kuifikisha Mauritania kwa mara ya kwanza katika fainali za AFCON msimu wa 2021/22. Gomez alikuwa anaifundisha klabu ya Al-Taraji ya nchini Saudi Arabia. Gomez amewahi kupita kwenye klabu mbalimbali Africa ikiwemo Simba, Coton Sport, El Merreikh na nyingine hivyo ana uzoefu na soka la Afrika kwa wastani mkubwa.

Makala Nyingine

More in International Football