Connect with us

NBC Premier League

KIPIGO CHA CHANGANYA WACHEZAJI SIMBA.

Simba imeburuzwa na klabu ya Yanga katika mchezo wa Derby kwa jumla ya magoli 1-5,wachezaji wa Simba walitokwa na machozi baada ya kushuhudia kipigo hicho.

Klabu ya Simba kwa mara ya kwanza imekubali kichapo katika mchezo wa Ligi kuu Kandanda Tanzania Bara walipokutana na Yanga November 5, 2023. Kabla ya hapo Simba msimu huu katika mashindano yote ilikuwa haijapoteza mchezo wowote [ AFL, Champions League, Ligi Kuu], ilikuwa imecheza ,ichezo sita (6) ya Ligi bila kupoteza.

Leo mbele ya Yanga, Simba imekubali kichapo kizito cha goli 1-5 ikiwa mwenyeji wa mchezo katika dimba la mkapa Jijini Dar Es Salaam, huu unakuwa ni mchezo wa kwanza klabu hiyo kukubali kipigo kizito namna hii kutoka kwa mtani wake Yanga.

Baada ya Mchezo kumalizika nahodha wa kikosi cha Simba Mohamed Hussein alisema mbinu walizoingia nazo ili kuizuia Yanga ziligoma baada ya Yanga kubadili mfumo wake na ikawapa ugumu kuikabili klabu hiyo.

Tulikuja na mpango wa kuwazuia wapinzani wetu pembeni zaidi maana mpira wa Yanga wanapenda kutumia sana mawinga. Lakini mchezo ulivyoanza tuliona mpango wetu umeharibika baada ya Yanga kuanza na Viungo wengi zaidi tuligundua hilo tukiwa uwanjani, hivyo ikatuwia ugumu kukabiliana nao. Tumepoteza mchezo wa Leo muhimu,tunajipanga na mechi zinazokuja.

Mohamed Hussein, Nahodha wa kikosi cha Simba baada ya kichapo cha 1-5.

Nahodha wa kikosi cha Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto baada ya ushindi huo mzito alisema Simba ilikuwa bora lakini wao walikuwa bora zaidi yao.

Tumepata ushindi mkubwa katika mechi kubwa. Mpinzani wetu alikuwa bora ila sisi tulikuwa Bora zaidi yao hii Leo ususani kipindi Cha pili. Baada ya kupata goli la kwanza na kukaa kidogo na wapinzani kurudisha tulipata funzo.

Wakati wa mapumziko tulijadiliana kulinda kwanza goli,maana wapinzani wetu ni bora kama sisi tulivyo bora. Derby hii ni kubwa ila Leo mtani kapunguza ladha ya ukubwa.”

Bakari Mwamnyeto, Nahodha wa klabu ya Yanga.

Mfungaji wa magoli mawili ya Yanga kati ya matano yaliyofungwa na timu hiyo amewaahidi mashabiki wa Yanga na wapenzi wa klabu hiyo kuwa wataongeza zaidi mazoezi ili waweze kubeba ubingwa.

Mechi ya derby ni mechi kubwa sana na ina presha sana ndani yake. Kupata ushindi wa goli Tano sio kitu kidogo katika mechi kubwa kama hii.

Kipindi Cha kwanza,sikuonekana sana kwasababu kila Timu ilikuwa juu wachezaji tunafikana sana miguu na mwilini na pia ukizingatia presha ilikuwa juu. Ukiangalia takwimu ya Yanga inapata magoli mengi kipindi Cha pili,dk 45 za pili tulikuwa kiutofauti sana.

Namshukuru Mungu Sina kikubwa Cha kuwahaidi mashabiki na wapenzi wa Yanga ila mawaambia tutaongeza zaidi mazoezi ili kushinda vikombe.

Max Nzengeli, mfungaji wa magoli mawili ya Yanga.

Klabu ya Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kufikisha alama 21 huku Simba ikisalia katika nafasi ya tatu (3) na alama zake 18, huku ikisalia na mchezo mmoja mkononi.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Max Nzengeli (2), Aziz Ki (1), Pacome (1) na Kenedy Musonda (1), upande wa Simba goli la kufutia machozi lilifungwa na Kibu Denis (1).

Makala Nyingine

More in NBC Premier League