Connect with us

NBC Premier League

SINGIDA YAWACHAPA MASHUJAA NYUMBANI.

Singida Fountain Gate imeichapa Mashujaa ya Kigoma magoli 1-3 katika uwanja wa Lake Tanganyika hii leo wakati Geita Gold ikitoshana nguvu na Tabora United.

Leo michezo miwili ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imefanyika katika viwanja viwili tofauti nchini Tanzania, Michezo yote imefanyika saa 10:00 Jioni kwa saa za Afrik Mashariki.

Dimba la Lake Tanganyika mkoani kigoma lilishuhudia mchezo mkali na wa kusisimua kati ya mwenyeji wa mchezo huo klabu ya Mashujaa dhidi ya Singida Fountain Gate mchezo uliomalizika kwa Singida Fountain Gate kuibuka na ushindi wa goli 1-3.

Magoli ya Singida Fountain Gate yamefungwa na Gadiel Michael dakika ya 18 kwa mpira wa kutenga alioupiga moja kwa moja, Marouf Tchakei dakika ya 44, na Habibu Kyombo dakika ya 64, goli la kufutia machozi kwa upande wa Mashujaa limefungwa na Adam Adam dakika ya 85 ya mchezo.

Matokeo hayo yameifanya Singida Fountain Gate kukwea hadi nafasi ya saba (7) kwenye msimamo ikiwa na alama 12 na kuiacha Mashujaa katika nafasi ya kumi (10) ikiwa na alama nane (8).

Mchezo mwingine ulioshuhudiwa leo ulikuwa ukiihusisha Geita Gold mwenyeji wa mchezo huu dhidi ya Tabora United mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kwa matokeo hayo Tabora United inashuka hadi nafasi ya tisa (9) ya msimamo wa Ligi ikikusanya alama 11 hadi hivi sasa huku pia Geita Gold ikiendelea kusalia katika nafasi ya 15 ya msimamo na alama saba (7) katika michezo tisa (9) waliyocheza.

Huu ni msimamo namna ulivyo hadi hivi sasa:

Makala Nyingine

More in NBC Premier League