Connect with us

Simba

SIMBA IFANYE MABADILIKO YA VIONGOZI.

Kocha wa za,ami wa klabu ya Simba Patrick Aussems aliwahi kusema kuwa ili Simba iweze kukua inapaswa kufanya mabadiliko ya viongozi.

Maoni na mitazamo imekuwa mingi sana baada ya kuondoshwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba Roberto Oliviera kutokana na matokeo aliyoyapata ya kufungwa goli 1-5 dhidi ya mtani wake wa jadi kllabu ya Yanga wakihuanisha na makocha waliopita.

Disemba 3,2019 aliyewahi kuwa kocha wa Simba Patrick Aussems aliandika ujumbe wa kuwashukuru na kuwaaga wapenzi, mashabiki wa Simba na Watanzania kwa ujumla kwa wakati wote waliokuwa pamoja baada ya kufutwa kazi na klabu hiyo. Sehemu ya ujumbe wake Aussems maarufu UCHEBE aliandika,

Ili simba ikue ni lazima iwaondoe kabisa Viongozi waongo na watu wasio na elimu kwenye bodi.

Aliandika Patrick Aussems.

Huenda ulikuwa ni ujumbe uliochukuliwa poa lakini kwa haya yanayoendelea sasa ya mashabiki na wapenzi kushinikiza mitandaoni baadhi ya viongozi wa juu wa klabu kuachia ngazi moja kwa moja linatukumbusha ujumbe wa Aussems ile Disemba 2019.

Makala Nyingine

More in Simba