Connect with us

CAF Champions League

VIINGILIO VYAWEKWA WAZI SIMBA VS ASEC.

Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kikosi chao kinaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas, mchezo utakaopigwa November 25, saa 10:00 Jioni katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam, Ahmed amemtaja nyota wao Aubin Kramo kuwa ataendelea kukosekana kuelekea mchezo huo.

Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu.

Ahmed Ally, Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba akizungumzia hali ya majeruhi kwenye kikosi chao.

Kwa upande mwingine Ahmed amewataja mashabiki wa klabu hiyo kuwa wageni rasmi wa mchezo huo mkubwa wa kimataifa. Huu umekuwa utaratibu wa klabu hiyo kutangaza wageni rasmi kuelekea michezo mikubwa wakianza na mchezo waliopoteza kwa goli 5-1 mbele ya mtani wao Yanga walipomtambulisha mchezaji wao Kibu Denis kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo.

Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.

Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.

Ahmed Ally akizungumzia kuhusu wageni rasmi wa mchezo.

Ahmed Ally pia ameweka wazi kuwa wageni wao klabu ya Asec Mimosas inatarajiwa kuingia nchini Novemba 23 kwajili ya mchezo huo mkubwa Barani Afrika, ikumbukwe Asec Mimosas waliondoshwa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Barani Afrika msimu uliopita na Bingwa wa mashindano hayo klabu ya USM Algers.

Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri.

Ahmed Ally aliongeza.

Kwa upande mwingne tayari klabu ya Simba imetangaza kiingilio cha mchezo huo kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo watakaoenda kuushuhudia mchezo huo mkubwa nchini.

Viingilio vya mchezo huu ni;
Mzunguko – Tsh. 5,000.
VIP C – Tsh. 10,000.
VIP B – Tsh. 20,000.
VIP A – Tsh. 30,000
Platinum – Tsh. 150,000.

Ahmed Ally alizungumza.

Klabu hiyo pia imetangaza kuwa ipo mbioni kumpata kocha mpya wa kikosi hicho lakini kwasasa kinaendelea na mazoezi tangu Jumatatu kikiwa chini ya kocha wa muda Daniel Cadena na Suleiman Matola.

Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.

Tupo katikati ya mashindano lazima tutafute kocha ambaye yupo active, atakuwa tayari kuanza majukumu ili akifika kazi ianze.

Ahmed Ameongeza.

Kauli mbiu kuelekea mchezo huo ni TWENDENI KINYAMA, MASHABIKI BOMBA.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League