Klabu ya Everton inayoshiriki Ligi kuu soka nchini England imekatwa alama kumi (10) baada ya kuvunja sheria ya matumizi ya pesa kupita kiasi kwenye usajili wa wachezaji wake [FFP RULES].
Baada ya kutolewa hukumu hiyo klabu ya Everton sasa imeshuka nafasi tano kwenda chini hadi nafasi ya 19 ya msimamo wa Ligi kuu soka England ikiwa na alama nne huku pia ikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa na klabu ya Burnley.
Everton wamevunja sheria baada ya kupata hasara ya £124.5 Million kwa msimu wa 2021/22, ikivuka kiwango stahili cha £105 Million kwa mwaka mmoja, na ina kuwa timu ya kwanza ya England kukatwa alama kwa kuvunja sheria za FFP.
Baada ya adhabu hii wametoa waraka wakitaka kukata rufaa kuhusiana na maamuzi hayo wakidai kuwa hawajatendewa haki.
Klabu ya Everton imeshtushwa na imefedheheshwa na uamuzi wa tume ya Ligi kuu. Klabu inaamini kuwa tume imetoa vikwazo vya michezo visivyo na uwiano na visivyo vya haki. Tayari klabu imeonyesha nia ya kuyakatia rufaa maamuzi kwenye bodi ya Ligi kuu.
Hatua za kukata rufaa sasa zitaanza na kesi hii itasikilizwa na bodi ya rufaa iliyoteuliwa kwa mujibu wa kanuni za Ligi kuu kwa wakati ufaao.
Everton inaamini ilikuwa wazi na huru kwenye taarifa zake ambazo ilitoa kwenye bodi ya Ligi na iliheshimu mchakato mzima ulivyokuwa unaenda.
Waraka wa Everton ulisomeka hivyo.
Manchester City walipambana na makosa 115 kutoka FFP ambayo msimu uliopita na yalipewa kipaumbele zaidi kwenye na tume ya Ligi kuu soka England.
Ni timu mbili pekee kutoka nchini England ambazo zimewahi kukumbana na adhabu ya kukatwa point, ilianza Middlesbrough msimu wa 1996-97 kwa kushindwa kutokea kwenye mchezo dhidi ya Blackburn.
March 2010, Portsmouth iliondolewa alama tisa (9), timu zote mbili zilishuka daraja baada ya kukatwa point hizo.
Sean Dyche ameshinda michezo minne (4) kati ya 12 ambayo ameiongoza klabu hiyo msimu huu lakini kwa sasa wapo nafasi ya 19.
Mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Jamie Carragher amesema adhabu hiyo imepitiliza kwa Everton.
Kuindolea Everton point kumi (10) ni adhabu kubwa sana na sio haki na ukizingatia wamecheza Ligi kuu kwa miaka mingi.
Jamie aliitumikia klabu hiyo utotoni.
Kuiondolea alama kumi (10) Everton kutaleta shauku ya kutaka kujua kama klabu zingine pia zitakumbana na adhabu kama hiyo.