Connect with us

Simba

YANGA KUSAJILI KIUNGO WA MPIRA JANUARY.

Klabu ya Young Africans imeanza mazungumzo na klabu ya Mtibwa Sugar kwaajili ya kuinasa saini ya nyota wake Ladack Chasambi mwenye umri wa miaka 19. Klabu ya Yanga inatarajiwa kukutana na upinzani mzito kutoka kwa klabu ya Simba ambayo pia imebisha hodi kwa walima miwa hao kutaka kuinasa saini ya nyota huyo.

Simba na Yanga wote wamegonga hodi Mtibwa Sugar kutaka kumsajili Ladack Chasambi. Tumeshawatajia dau la mchezaji wetu mwenye mkataba, kwahiyo wajipange waje mezani tumalizane.

Afisa mtendaji mkuu wa Mtibwa Sugar, Swabri akizungumza.

Chasambi amelelewa kwenye kikosi cha vijana cha klabu ya Mtibwa Sugar, ameitumikia Mtibwa Sugar katika timu zote za vijana za klabu hiyo kwenye mashindano yote, amecheza U15, U17, U20 na U23 na ni mchezaji bora mara mbili mfululizo wa ligi ya Vijana chini ya miaka 20 misimu miwili mfululizo 2021/22, 2022/23.

Tangu msimu uliopita nyota huyo amepandishwa kuitumikia timu ya wakubwa ya Mtibwa Sugar katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo inashiriki.

Ladack anavutiwa zaidi kufanya kazi na Max Mpia Nzengeli nyota wa klabu ya Yanga lakini pia anavutiwa na namna nyota huyo anavyojituma awapo uwanjani. Huenda dirisha dogo la usajili la mwezi January likawakutanisha nyota hawa na kufanya kazi pamoja.

Kama atajiunga na Young Africans basi ataungana na nyota wengine waliotoka kwenye mashamba ya miwa mkoani Morogoro kama golikipa wa sasa wa Yanga Abutwalib Mshery, Dickson Job na Kibwana Shomari lakini kama atajiunga na Simba pia atakutana na nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar Mzamiru Yassin.

Kwasasa Ladack Chasambi yupo na timu ya Taifa ya Tanzania inayocheza mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Niger hii leo nchini Morocco.

Makala Nyingine

More in Simba