Klabu ya Everton inatarajia kukutana rugu lingine la kukatwa alama 9 iwapo wamiliki wapya wa klabu hiyo kampuni ya 777Partners watashindwa kulipa kiasi cha £ 300 Million kwa klabu za Leeds United, Leicester City pamoja na Burnley baada.
Timu hizo tatu zinajiandaa kuwasilisha malalamiko ili zilipwe kiasi cha £100 Million kila klabu baada ya kushuka daraja kwa miaka ya hivi karibuni.
Kama klabu hiyo itashindwa kuzilipa Leeds United, Burnley na Leicester City basi itakutana na adhabu hiyo ya kukatwa alama tisa (9).
Leicester inalalamika kuwa Everton ilistahili kukatwa alama msimu uliopita, alama ambazo zingeishuhudia Everton ikishuka daraja na Leicester City ikisalia kwenye Ligi kuu kandanda England msimu huu.
Kama timu hizo zitashinda kesi basi Everton italazimika kulipa fidia ta £300 Million. Ni wazi kuwa wamiliki wapya wa Everton 777partners hawataweza kuilipa fidia hiyo na hivyo klabu hiyo itaondolewa alama zingine tisa (9).
Hii inakuja baada ya Everton kuondolewa alama kumi (10) kutokana na matumizi ya pesa kupita kiasi na kuvunja sheria ya FFP.
Inaaminika kuwa tayari Leeds, Leicester City na Burnley wamewasiliana na 777Partners kabla ya kuwasilisha malalamiko yao kwenye mamlaka ya Ligi kuu soka nchini England ili ifanye utambuzi kama watapatikana na hatia.
Burnley ilishuka daraja 2022 kufuatia Everton kutumia matumizi makubwa ya pesa yaliyoisaidia klabu hiyo kumaliza na alama nne mbele ya mstari wa kushuka daraja.
Leeds na Leicester City ambazo zilishuka daraja msimu uliopita, zinalalamika kuwa Everton ilitakiwa kupokonywa alama msimu wa 2022/23, msimu ambao walisalia kwenye Ligi kwa tofauti ya alama mbili kutoka timu iliyoshuka daraja.
Klabu zote mbili sasa zina siku 28 za kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka ya Ligi kuu nchini England na mamlaka hiyo inatarajia kusikiliza malalamiko hayo kabla ya msimu huu kumalizika.
Kama Everton ikitiwa hatiani italazimika kuwauza nyota wake wenye majina makubwa akiwemo Jordan Pickford na Dominic Calvert-lewin.
Hii sasa itaipelekea Everton kuendelea kusalia kwenye nafasi ya timu zinazoshuka daraja licha ya kuwa Super Computer imeeleza kuwa klabu hiyo itasalia Ligi kuu msimu huu hata baada ya kuondolewa alama kumi (10) za mwanzo.
Klabu ya Chelsea na Mnchester City pia zinaweza kuwa kwenye eneo la kushuka daraja kama zikikutwa na hatia na FFP kama ilivyokuwa kwa klabu ya Everton. City walikutwa na makosa 115 mwaka uliopita.