Connect with us

EPL

MANCHESTER UNITED KUIKOSA UEFA MSIMU UJAO.

Klabu ya Manchester United huenda ikashindwa kushiriki Ligi ya mabingwa Barani Ulaya msimu ujao kama dili la Jim Ratcliff la kuwa na hisa kwenye klabu hiyo litakamilika.

Sheria za UEFA zinaeleza kuwa timu mbili zilizo chini ya umiliki wa mtu mmoja haziwezi kushiriki shindano moja. Ineos ina sehemu ya umiliki kwenye kikosi cha NICE kinachoshiriki Ligi kuu nchini Ufaransa na ipo nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi hivi sasa.

Sheria za UEFA zinasema kama ikitokea klabu mbili zinamilikiwa na kampuni moja basi timu moja itakayomaliza nafasi za juu kuliko timu nyingine itapata nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya na nyingine itakosa.

Kma NICE itamaliza nafasi ya juu zaidi ya United basi itapata nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA, na kama Manchester United itamaliza nafasi ya juu zaidi ya NICE basi itapata nafasi ya kushiriki UEFA na Nice itasalia kushiriki Ligi kuu pekee.

Mfano: Manchester United ikimaliza nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi England na NICE ikamaliza nafasi ya pili au ya tatu Ufaransa basi Nice itashiriki UEFA na Man U itabaki kushiriki Ligi ya ndani pekee.

Njia pekee kwa Manchester United ili ishiriki UEFA basi ni kubeba Carabao Cup mashindano ambayo tayari imeshaondoshwa na isimalize kwenye nafasi ya juu inayomuwezesha kushiriki UEFA lasivyo haitashiriki hata ikibeba kombe la Ligi.

Makala Nyingine

More in EPL