Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amefichua juu ya kile ambacho kilizungumzwa kwenye kikao kati ya viongozi wa klabu ya Simba SC na wachezaji wake mara baada ya mchezo wa kwanza wa makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika waliolazimishwa sarenyumbani na Asec Mimosas
Baada ya mchezo wetu dhidi ya Asec Mimosas ambapo matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wetu na huo unaweza ukawa mwendelezo wa matokeo mabaya ya Mnyama Simba SC.
Kama Simba Sc ikatulazimu jana kukutana kwa ajili ya kujifanyia tathimini na kuulizana kwani tunakosea wapi kwa sababu huu sio mwenendo wa kawaida kwenye timu kama ya Simba Sc, kwa sababu ukiangalia tayari tuna michezo mitatu ambayo yote hatujapata ushindi
Alisema Ahmed Ally.
Vilevile Ahmed Ally amesema kikao hicho hakikulenga kunyosheana vidole, au nani kafanya nini bali ni kujadili changamoto mbalimbali zinazopelekea timu hiyo kukosa muendelezo wa kufikia malengo ambayo taasisi kubwa kama Simba SC inashindwa kuyafikia.
Ikabidi tukutane jana pale Kambini kwetu Mbweni kuzungumza wachezaji na benchi la ufundi, wachezaji wazungumze na viongozi viongozi wazungumze na benchi la ufundi ili tuweze kung’amua kuna shida gani hapo katikati ambayo inatufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu ipasavyo.
Na kweli kikao kilikuwa very successful wachezaji wakazungumza viongozi wakazungumza na hakikuwa kikao cha kutafuta mchawi wala kunyoosheana vidole kilikuwa kikao cha kujifanyia tathimini jamani kwanini inakuwa hivi.
Alimaliza kwa kusema hivyo msemaji wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally.
Ikumbukwe Simba SC ipo katika kipindi kigumu hasa msimu huu ambapo mpaka sasa hawajafanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika michuano ya kimataifa. Walianza kwa sare ya mabao 2-2 na Power Dynamos ugenini Zambia, kisha wakalazimisha sare ya 1-1 kwenye mchezo wa marudiano katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar Es Salaam.
Huku kwenye michuano mipya kabisa barani Afrika African Football League (AFL), ambayo ilianzia katika hatua ya robo fainali Simba SC walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na klabu ya Al Ahly kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulichezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa na baadae kulazimishwa tena sare ya bao 1-1 ugenini nchini Misri.
Sare dhidi ya Asec Mimosas imewastua viongozi na kuamua kuitisha kikao ili kuinusuru timu hiyo na maneno mabaya ya mashabiki kwa kushinikiza viongozi wajiuzuru, huku wengine wakionekana kuisusia timu na kutokwenda kuishangilia timu hiyo pindi itakapokuwa ikishuka dimbani katika mechi mbalimbali.