Connect with us

NBC Premier League

TATHMINI KABLA YA MCHEZO : AZAM V KMC

Pengine Azam wanapitia nyakati bora zaidi za msimu huu hivi sasa, Kocha wao Bruno Ferry akitwaa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi lakini Kiungo wao Feisal Salum akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi.

Ushindi wa asilimia 100 ndani ya mwezi, Wakiwanyuka Mashujaa 3-0, Ihefu 3-1 na kuifumua vilivyo Mtibwa Sugar  5-0, wakifunga  magoli 11 na kuruhus bao 1 tu, Azam wapo mawinguni.

Ushindi dhidi ya KMC leo utawafanya Azam kukwea kileleni mwa msimamo kwa muda wakiishusha Yanga wakiwa na michezo zaidi wamecheza lakini haitojalisha, kikubwa watakuwa namba 1 kwenye msimamo baada ya kuwa na nyakati kadhaa ngumu siku kadhaa nyuma hivyo watauchukulia mchezo wa leo kwa uzito mkubwa sana wakijua ushindi una maana gani kwenye malengo yao ya msimu huu.

Kocha Moalin siyo mgeni kwenye viunga hivi vya Chamazi, anaifahamu Azam FC lakini anajua pia sio Azam ile aliyoiacha akiwa na vijana wake wa sasa hivi akina Tepsie Evans. KMC wanajiandaa kutoa upinzani hata hivyo.

Lakini kama kuna namna yoyote KMC watahitaji kupata matokeo leo dhidi ya Azam basi watahitaji kuongeza bidii zaidi ya waliyoionyesha dhidi ya Mashujaa, kwani licha ya kushinda 3-2 lakini hawakucheza vizuri.

KMC bila shaka nao wapo kwenye mbio za kusaka nafasi 4 za juu kwa nafasi waliyopo badao wana uwezo wa kufikia malengo yao nap engine wanaweza kuyaweka hai kwa kupata ushindi dhidi ya Mtajiri hawa wa Chamazi ambao wameonekana kuwa wa motto sana.

WA KUANGALIWA :

AZAM FC : FEISAL SALUM ; ukiachana tu kufunga magoli, Fei Toto amehusika kikamilfu kabisa kwa asilimia 90 ya magoli yote ya Azam Fc msimu huu, amekuwa bora sana na hata tuzo aliyopewa mwezi huu sio bahati mbaya

KMC : ABDIKARIM QUBAAYE; Tangu ajiunge na KMC ameendelea kummpa sababu Kocha Moalin Kumuamini na mra kadhaa imemmlipa. Moja ya viungo bora sana pale KMC na amehusikam kwenye mgoli ya KMC kwa zaidi ya asilimia 50 msimu huu.

MUDA WA MECHI : SAA 3 USIKU

UWANJA : AZAM COMPLEX

Makala Nyingine

More in NBC Premier League