Connect with us

NBC Premier League

KMC YATAMBULISHA JEZI MPYA ZA MAZOEZI.

Klabu ya KMC inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara leo imetambulisha rasmi jezi watakazozitumia kwenye uwanja wa mazoezi msimu huu.

Mashabiki wengi wamezifananisha jezi hizo na zile zinazotumiwa na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Hawa ni masandawana wa Dar Es Salaam, mmetoa jezi nzuri sana.

Shabiki mmoja aliandika kwenye ukurasa wa klabu hiyo.

Klabu hiyo kwasasa ipo mkoani Arusha, Wilaya ya Karatu kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara dhidi ya Singida Fountain Gate ambao wanatumia uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu kama uwanja wake wa nyumbani.

Ikumbukwe Singida Fountain Gate ilifungiwa kuutumia uwanja wa CCM Liti kutokana na kutokukidhi mahitaji ya kucheza michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League