Klabu ya Simba inashuka dimbani hii leo kuikabili Wydad AC katika mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Huu ni kama mchezo wa fainali kwa timu zote mbili kwani kila mmoja anahitaji zaidi kupata matokeo katika mechi hii ili impe mwanga wa kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali.
Wydad AC imecheza na Simba mara tatu [3], na michezo yote imefanyika ndani ya mwaka huu, ikiwa miwili [2] ni ya michuano ya African Football League na mmoja [1] wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
- Simba imeshinda mchezo mmoja [1] kati ya mitatu [3].
- Simba imefunga goli moja [1] pekee katika michezo hiyo mitatu [3].
- Simba haijawahi kupoteza mchezo wowote katika uwanja wa Benjamini Mkapa dhidi ya Wydad AC.
- Katika michezo hiyo mitatu Simba imeonyeshwa kadi za njano sita [6].
- Hadi hivi sasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, Simba haijapata ushindi wa aina yoyote katika michezo mitano [5] iliyopita, ikiwa imepoteza mchezo mmoja [1] pekee na sare nne [4].
- Katika michezo saba [7] iliyopita katika mashindano yote Simba imefunga magoli nane [8] na kufungwa magoli tisa [9].
- Wydad AC imeshinda michezo miwili [2] kati ya mitatu [3] iliyocheza dhidi ya Simba.
- Imefunga magoli mawili [2] pekee kwenye mechi zote tatu [3].
- Wydad AC imeshinda michezo yote ikiwa nyumbani kwao, haijawahi kushinda ikiwa uwanja wa Mkapa.
- Katika michezo mitatu iliyocheza dhidi ya Simba, Wydad imeonyeshwa kadi za njano nane [8].
- Katika michezo mitano [5] iliyopita, Wydad AC imeshinda michezo mitatu [3] na kupoteza michezo miwili [2] katika mashindano yote.
- Wydad AC imefunga jumla ya magoli sita [6] na imefungwa magoli matano [5].
Kituo kinachofuata ni Benjamin Mkapa, leo saa kumi Alasiri [16:00] huku kila timu ikiwa na kocha mgeni baada ya Wydad AC kumtimua kazi Adil Ramzi kutokana na matokeo yasiyoridhisha iliyoyapata timu hii hivi karibuni.