Connect with us

CAF Champions League

ONANA AMTAJA BENCHIKHA SABABU YA UBORA WAKE.

Klabu ya Simba inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na Ligi ya mabingwa Afrika msimu huu, jana iliibuka na ushindi wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa [2-0] dhidi ya Wydad AC.

Magoli yote mawili ya Simba yalifungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Cameroon Willy Essomba Onana ndani ya dakika mbili za kipindi cha kwanza.

Haya yanakuwa magoli ya kwanza kwa nyota huyo kuifungia timu yake katika michezo ya kimataifa tangu alipojiunga na klabu ya Simba mapema kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu.

Baada ya ushindi huo mfungaji wa magoli yote mawili Willy Essomba Onana alisema hakuna siri yoyote ile lakini ni wakati wa Mungu tu ndio umefika na ndio maana amefunga goli mbili na kuisaidia timu kupata alama tatu [3] za kwanza za mashindano hayo.

“Hakuna siri yoyote ni Mungu tu, kama ni wakati wako ni wako tu, namshukuru sana Mungu na kocha kwasababu amenijenga kujiamini”.

“Nitoe pongezi pia kwa timu kwasababu huu ni ushindi kwaajili ya timu, tulicheza kama timu na tukashinda kama timu”.

“Mashabiki wametupa nguvu kubwa sana leo, kwahiyo tunawaomba mashabiki wawe wanajitokeza kutushangilia”.

“Kuna wakati timu inapitia wakati mgumu, lakini wakati ambao kila kitu hakipo sawa ndio wakati wa kujua nani shabiki wa kweli, tunahitaji mashabiki wa kweli”.

“Natumaini kwenye mchezo unaofuata tutakuwa na mashabiki wengi watakaojitokeza uwanjani”.

  • Leandre Willy Onana – Mfungaji wa magoli mawili ya Simba.

Klabu ya Simba sasa inashika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi B ikiwa na alama tano [5] nyuma ya Asec Mimosas iliyo na alama kumi [10] na tayari imefuzu hatua inayofuata ya robo fainali.

Simba imesalia na michezo miwili ili kukamilisha michezo sita [6] ya kundi, mmoja watacheza nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy na mwingine watacheza ugenini dhidi ya Asec Mimosas.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League