Baada ya uwanja wa Uhuru kufungiwa kwasababu za kutokukidhi viwango vya ubora ambavyo vinahitajika kwenye michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara, mchezo baina ya KMC na Simba sasa utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Simba na KMC zinatarajiwa kushuka dimbani hapo kwesho kwenye mwendelezo wa michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.
Klabu ya Simba itakuwa ugenini katika mchezo huo kuikabili KMC ambayo asilimia kubwa ya michezo yake ilikuwa inautumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wake wa nyumbani.
- Timu hizi zimekutana mara kumi [10] na mara tisa [9] klabu ya Simba imeshinda na kutoa sare mchezo mmoja [1], KMC haijawahi kupata ushindi wa aina yoyote mbele ya klabu ya Simba.
- Simba imeifunga KMC magoli 23 na imefungwa magoli saba [7].
- Mchezo ambao ulihusisha magoli mengi uliisha KMC 1-4 Simba.
- Timu hizi zikikutana KMC ikiwa nyumbani mchezo huwa unazalisha magoli mawili [2+] na kuendelea, mchezo mmoja pekee uliozalisha goli moja ambao Simba ilikuwa nyumbani, mchezo huo ulimalizika kwa Simba 1-0 KMC.
- Katika michezo mitano [5] iliyopita ya Ligi msimu huu klabu ya Simba imeshinda michezo mitatu [3], imetoa sare mchezo mmoja [1] na kupoteza mchezo mmoja [1], ipo nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi.
- KMC katika michezo yake mitano [5] ya Ligi iliyopita, imeshinda mchezo mmoja [1], sare michezo miwili [2] na kupoteza michezo miwili [2], ipo nafasi ya tano [5] ya msimamo wa Ligi.
Kesho majira ya saa 10:00 Jioni timu hizi mbili zitashuka dimbani katika uwanja wa Azam Complex Jijini Dar Es Salaam kwaajili ya mwendelezo wa michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.