Connect with us

Mapinduzi Cup

SIMBA KUMALIZANA NA APR MAKUNDI LEO

Simba SC wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi, Kundi B wakimenyana na APR ya Rwanda.

Klabu zote mbili zimetoka kushinda michezo yao ya Mwisho, APR wakishinda 3-1 dhidi ya JKU huku Simba wakipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida FG.

Simba wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 6 baada ya michezo yao miwili[2] wakifuatiwa na Singida FG wenye alama 6 pia baada ya mechi zao 3.

APR wanashika nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 3 walizovuna baada ya mechi 2.

Ugumu wa Mechi ya leo unachagizwa na umuhimu wa alama 3 kwa timu zote mbili ikizingatiwa kuwa wote wanawania nafasi ya kufuzu bado.

Japokuwa Simba wamejiwekea uhakika mkubwa wa kufuzu Robo Fainali lakini kumaliza nafasi ya kwanza wakiwa na alama zote 9 ni heshima kwao hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili huku Heshima pia ikiwa kwenye ajenda.

Ili APR wafuzu moja kwa moja Robo Fainali ni lazima waifunge Simba zaidi ya goli 3 ili waivuke Singida FG lakini pia ipo Fursa ya kufuzu kama Washindwa Bora endapo watashinda kwa ushindi chini ya hapo, Sare au pengine hata wakipoteza zikiangaliwa takwimu za michezo ya makundi mengine.

Kocha Thierry Froger wa APR alisema kuwa anafahamu ana mchezo mgumu kiasi gani kuwakabili Simba kwakuwa ni timu kubwa Afrika lakini watapambana kupata ushindi dhidi yao.

Mechi hii inatarajiwa kupigwa majira ya saa 2.15 usiku.

Makala Nyingine

More in Mapinduzi Cup