Connect with us

Mapinduzi Cup

SIMBA YASHINDWA KUTAMBA KWA APR

Simba imelazimishwa suluhu ya 0-0 na APR kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B la michuano ya Mapinduzi Cup.

Kama ilivyokuwa kwa Kocha Benchikha kwenye kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kwenye kila mchezo ndivyo ilivyo kwa Kocha Thierry Froger. Timu zote zilifanya mabadiliko makubwa kwenye vikosi vyao kuanzia wachezaji hadi mifumo, huku Simba wakimkaribisha Michael Charamba.

Mchezo ulianza kwa umakini zaidi kwa timu zote lakini Simba walionekana kuwa kwenye utulivu zaidi wakicheza kwa kugongeana kuanzia chini bila ya kuwa kwenye shinikizo lolote. Iliwalizimu APR kuukimbiza zaidi mpira.

Matatizo ya kimawasiliano kati ya Hussein Abel na mabeki wake katika kuondoa mpira wa krosi uliopigwa na Bosco Ruboneka nusura yawagharimu kwani mpira ulimdondokea Sharaf Eldin Shaiboub lakini kichwa chake kiligonga nguzo.

Shuti la kulenga lango la kwanza la mchezo lilipatikana dakika ya 27 ya mchezo baada Christian Ishimwe kuingia na mpira kwenye eneo la hatari la Simba lakini shuti lake lilipanguliwa vema na Hussein Abel.

Saido Ntibazonkiza alijitengenezea nafasi ya kupiga kutokea upande wa kushoto lakini shuti lake lilitoka nje sentimita chache.

Mpira wa kona uliochongwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya 44 ulitua kichwani kwa Jimmyson Mwanuke lakini mpira wake ulidakwa kwa umaridadi kabisa na Pavelh.

Dakika ya 45+3, APR walijibu kwa shuti kali la John Bosco Ruboneka lakini nalo pia liliishia kwenye mikono salama ya Hussein Abel.

Timu zote zilienda mapumziko zikiwa 0-0

Simba walirudi kipindi cha pili na mabadiliko, wakitambulishwa mchezoni Luis Miquissone na Willy Essomba Onana na Jean Baleke wakitoka Michael Charamba, Shabani Iddy Chilunda na Jimmyson Mwanuke.

Hussein Abel aliendelea kuiweka salama timu yake akiokoa mchomo wa mmoja kwa mmoja wa Taiba aliyepokea pasi akiwa peke yake na Gilbert Mugisha.

Simba walipata nafasi kupitia kwa Jean Baleke aliyepigiwa krosi nzuri na Saido Ntibazonkiza lakini kichwa chake kilikuwa hafifu na kudakwa kirahisi na golikipa Pavelh.

Timu zote zimeonekana kushambuliana kwa zamu na kuonyesha nia ya dhati ya kutafuta ushindi. Ila hutoacha kuisifu Safu ya ulinzi ya APR iliyokuwa imara sana kudhibiti mashambulizi mengi ya Simba.

Dakika zote 90 zikamalizika kwa suluhu ya 0-0. Matokeo haya yanaifanya timu ya APR kufuzu kama Mshindwaji Bora.

Makala Nyingine

More in Mapinduzi Cup