APR ya Rwanda imewaondosha mashindanoni Yanga kwenye michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kuwachapa kwa mabao 3-1 na kutinga nusu fainali.
Yanga walianza mchezo kwa kasi wakipeleka mashambulizi mfululizo kwa timu ya APR ambayo yenyewe iliamua kucheza chini kwa kuwaheshimu Yanga. Ni kama walijiwela hatarini sana kwa aina hii ya uchezaji kutokana na kasi wanayokuwa nayo Yanga wakati wanashambulia.
Farid Mussa alipata nafasi dakika ya 9 tu ya mchezo lakini shuti lake lilipanguliwa na golikipa Nzila Pavehl.
Yanga walipata kona iliyochongwa na Farid Mussa lakini kichwa cha Gift Fred kilipaa juu ya lango kidogo.
Mahlathe Skudu Makudubela alipata nafasi pembeni kidogo mwa lango pa APR lakini shuti lake lilibabatiza walinzi na kutoka nje kidogo ya lango. Kona haikuweza kuitumia vizuri.
Dakika ya 23 ya mchezo, Jesus Moloko aliitanguliza timu yake ya Yanga akitumia vema kazi nzuri iliyofanywa na Clement Mzize akitumia madhaifu ya mlinzi Banga kuushinda mpira na kutoa pasi kwa mfungaji. 1-0 kwa Yanga.
Yanga waliendelea kuutawala mchezo huku APR wakiwa nje kabisa ya mpango wao, zaidi ni namna ambavyo walielemewa kwenye eneo la kiungo kutokana na kuwa na viungo wachache wakabaji. Ni Salim Pitchou tu ndiye aliyekuwa kiungo mkabaji asilia. Bosco Ruboneka na Ramadhan Niyibizi wote ni viungo washambuliaji.
Wakati ikionekana Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0, APR walikuwa na mawazo tofauti. Pasi fupi ya Kibwana Shomari ilinaswa na Suley Sanda aliyempasia Victor akapiga shuti lililookolewa na Mshery lakini likamrudia Suley Sanda tena aliyeuiwamisha mpira kimiani na kufanya matokeo 1-1 dakika ya 45+4
Yanga walikwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu na APR kwa bao 1-1.
Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko wakiwaingiza Shekhan na Crispin Ngushi ili kuongeza kasi ya ushambuliaji.
Dakika ya 47 tu ya mchezo, APR walipata mkwaju wa penati baada ya Abutwalib Mshery kumfanyia madhambi Ndayishimiye kwenye eneo la hatari na muamuzi kuamuru adhabu hiyo. Victor Mbaouma hakufanya ajizi na kuukwamisha mpira nyavuni kuipa utangulizi timu yake. 2-1 kwa APR dakika ya 49.
Ni kama APR walirudi kwa kasi sana kipindi hiki cha pili wakiwanyima kabisa uhuru Yanga waliokuwa nao kipindi cha Kwanza. Kuingia kwa Sharaf Eldin Shaiboub eneo la kiungo paliwaweka hai sana APR kipindi hiki cha pili huku Taiba akiongeza kasi ya mashambulizi.
Yanga wakaonekana kutoka kwenye mchezo wao ikiwalazimu hivyo kutokana na kuwa nyuma kwenye matokeo, wakishindwa kujenga mashambulizi kiufasaha na kutumia zaidi mipira ya mbali.
Dakika ya 79, APR Walipata bao la 3 baada ya winga Taiba kufanya kazi nzuri kwenye eneo la hatari la Yanga na kupiga pasi ya kisigino ndani kwa Sharaf Eldin Shaiboub aliyeachia kiki kali kulia kwa Mshery kuitanulia timu yake uongozi. 3-1 kwa APR.
APR waliuchukua mchezo kuanzia hapa, Yanga ikawa timu ya pili kiwanjani. Wakiufukuza zaidi mpira lakini waliwakuta APR wamejizatiti eneo la ulinzi.
Shekhan Ibrahim alipata nafasi ya kupiga pigo huru nje kidogo ya eneo la APR Lakini golikipa Pavelh alikuwa sambamba nalo.
Dakika ya 88, Shekhan Ibrahim tena alijaribu mkwaju mwingine lakini safari hii shuti lake likagonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Yanga walijaribu kulisogelea lango la APR mara kadhaa lakini hawakuweza kufua dafu, APR wakiwa na umiliki wa mpira kwa asilimia 58.
Mpira ulimalizika kwa APR kuibuka na Ushindi wa mabao 3-1 baada ya dakika 90 zote kumalizika.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...