Simba wamefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya mashindano ya Mapinduzi Cup 2023 baada ya kushinda 3-2 kwenye changamoto za mikwaju ya penati kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 na sasa watacheza dhidi ya Mlandege kwenye Fainali.
Singida FG walipata nafasi ya mapema kabisa sekunde ya 45 tu kupitia kwa Elvis Rupia akiwa anatizamana na golikipa Ally Salim lakini alikosa lengo na shuti lake kupaa juu.
Dakika ya 11, Marouf Tchakei alitumia makosa ya Kennedy Juma kupiga pasi fupi na kuinasa kisha kumpasia Elvis Rupia aliyekuwa kwenye nafasi nzuri ya kupiga shuti kali lililomshinda Ally Salim na kujaa wavuni kuitanguliza timu yake. Singida FG 1-0 Simba.
Simba hawakuonekana kuwa na makali sana dakika hizi za kipindi cha kwanza, pakionekana hakuna mpango wa maana kiuchezaji wa kutengeneza nafasi za kufunga huku pia wakipoteza mipira.
Singida FG kwa upande waliendelea kuifaidi hali hii, wakitumia mwanya huu kutuliza timu huku wakishambulia kwa nyakati. Mara nyingi wakionekana Tchakei, Abuya na Kaseke wakipishana vema na kuongeza kasi kipindi wanashambulia. Lakini hutoacha kusifu mpango wao wa kuhakikisha Simba hawapati uhuru wa kucgeza.
Pakiwa hakuna matukio muhimu yaliyotokea, kwenye upande wa takwimu, Simba waliumiliki mchezo kwa aslimia 57 dhidi ya 43 za Singida FG huku wakipiga shuti 3 zilizolenga lango. Shuti 1 tu la Singida ndio limezaa bao pekee la dakika hizi.
Mapumziko, Singida FG walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Hussein Kazi na Moses Phiri walitambulishwa kwenye mchezo na Simba kipindi cha pili, wakichukua nafasi za Kennedy Juma na Jean Baleke.
Saido Ntibazonkiza alipiga piga la adhabu kubwa nje kidogo ya eneo la hatari la Singida FG lakini mpira wake ulienda kugonga mwamba wa pembeni. Dakika ya 55 bado ilikuwa 1-0 kwa Singida FG.
Dakika ya 60 Simba walimuingiza Luis Miquissone nafasi ya Babacar Saŕr ili kuongeza kasi ya mashambulizi wakirudi kwenye mfumo wao wa 4-2-3-1.
Singida FG walipata nafasi ya kupata bao la pili, pasi nzuri ya Marouf Tchakei kumpenyezea Kelvin Kijiri lakini alishindwa kutumia nafasi.
Simba wakajibu mapigo kupitia kwa Saido Ntibazonkiza akipata nafasi ndani ya kisanduku lakini shuti lake likaenda nje kidogo ya lango.
Daika ya 67 Simba walipata kona iliyochongwa vizuri na Essomba Onana, lakini kichwa cha Sadio Kanoute hakikulenga lango.
Singida FG wakati huu walifanya mabadiliko kumuingiza Hamadi Waziri kuchukua nafasi ya Kiungo Yusuf Kagoma. Mabadiliko ya kuimarisha safu ya ulinzi huku Meddie Kagere pia akichukua nafasi ya Elvis Rupia.
Willy Essomba Onana alipata majeraha na Mwalimu Benchikha kuamua kumpumzisha na kumuingiza Salehe Karabaka.
Marouf Tchakei alimpisha Amos Kadikilo dakika za mwishoni mwa mchezo ili kuongeza nguvu eneo la ulinzi.
Nidhamu kubwa ya Singida FG iliendelea kuwaweka salama kwani licha ya Simba kujaribu kujenga mashambulizi yao, waliwakuta Singida FG wako imara kwenye eneo la ulinzi.
Dakika za mwisho kabisa za mchezo huu, ikionekana mechi kama inamalizika kwa Singida FG kuibuka na ushindi, Fabrice Ngoma alitumia vizuri nafasi ya dhahabu aliyopata kutokana na mpira wa kona uliochongwa na Saido Ntibazonkiza, wakati walinzi wanaokoa ikamdondokea yeye na kuipa timu yake bao la kusawazisha. 1-1.
Mchezo ukalazimika kuingia hatua ya changamoto za mikwaju ya penati ambapo Simba walishinda kwa penati 3-2 Na kufuzu hatua ya fainali.
Waliopata penati upande wa Simba ni Luis Miquissone, Israel Mwenda, Moses Phiri huku Waliokosa ni Shomari Kapombe na Saido Ntibazonkiza.
Waliopata Penati upande wa Singida ni Duke Abuya na Deus Kaseke huku Waliokosa ni Gadiel Michael, Hamadi Waziri na Meddie Kagere
Mchezaji Bora wa Mchezo alichaguliwa kuwa Kelvin Kijiri wa Singida FG huku mchezaji mwenye nidhamu akichaguliwa kuwa Che Malone Fondoh wa Simba.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...