Connect with us

Makala Nyingine

RAIS CAF ATANGAZA KUFUTA KOMBE LA SHIRIKISHO.

Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika Patrice Motsepe ameweka wazi mpango uliopo wa kuyafuta mashindano ya kombe la shirikisho Barani Afrika kwa lengo la kupunguza idadi ya mashindano ambayo yanaonekana kuwa mengi.

Sababu nyingine ambayo inatajwa kusababisha michuano hiyo kufutwa ni pamoja na uhaba wa wadhamini hasa baada ya michuano mikubwa ya Ligi ya mabingwa Afrika kusumbuka kupata wadhamini wapya na hali ngumu ya kiuchumi kwa klabu zinazoshiriki.

Michuano hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2004 baada ya kuunganishwa kwa michuano miwili ya kombe la washindi [African Cup Winner’s] na kombe la CAF [Caf Cup].

Patrice Motsepe ambaye alichukua hatamu ya kuliongoza shirikisho la soka Barani Afrika mnamo mwezi March 2021 amewekeza nguvu kubwa katika kuboresha soka Barani Afrika. Chini ya uongozi wake michuano ya AFL imefanyika na bingwa akawa Mamelodi Sundowns.

“Tunaweza kuyafuta mashindano ya kombe la shirikisho, tuna mashindano mengi sana”.

“Hatutakuwa na hatuwezi kuwa na mashindano mengi, Ligi ya mabingwa ni nzuri tunahitaji kuilinda na kuipa nguvu zaidi”.

“Ndio maana sikuweka zawadi kubwa ya ushindi kwenye mashindano ya AFL ili kutafanya yawe zaidi ya Ligi ya mabingwa”.

“Sikutaka kutengeneza fikra kwamba katika hii hatua ghafla tu mashindano ya AFL ni makubwa zaidi ya Ligi ya Mabingwa”.

Kwa mujibu wa Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika, Patrice Motsepe mashindano ya kombe la shirikisho hayana mvuto kama Ligi ya mabingwa kitu ambacho kimezua gumzo kwa wadau wengi wa soka Afrika.

Wadau wengine wanaamini kuwa licha ya changamoto zilizopo kwenye mashindano ya kombe la shirikisho lakini yanatoa nafasi kwa maendeleo ya klabu na wachezaji kutoka mataifa madogo kushindana katika hatua kubwa.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine