Connect with us

AFCON

SERIKALI YAINGILIA KATI MATOKEO NIGERIA.

Baada ya kupata sare katika mchezo wa kwanza wa fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Equatorial Guinea maafisa kadhaa wa serikalini wamewafuata wachezaji ili kujua nini wana kiwaza kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast.

Hali imekuwa si shwari kwenye kambi ya Nigeria kutokana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wana matumaini makubwa na kikosi chao kwenye michuano hii.

Nyota wa timu hiyo Alex Iwobi amesema kuwa ni kawaida kuwepo kwa presha Nigeria isipofanya vizuri kwasababu mashabiki wana matumaini na kikosi chao.

“Hivyo ndivyo ilivyo Nigeria, kama msiposhinda basi ni hasara”, amezungumza Alex Iwobi.

Nigeria ndio timu iliyotazamiwa kufanya vizuri zaidi katika michuano hii kutokana na uwepo wa wachezaji wengi nyota na wanaofanya vyema Barani Ulaya akiwemo Victor Ohsimen.

Siku chache kabla ya fainali hizi kuanza mshambuliaji wa klabu ya Real Sociedad Umar Sadiq aliondolewa kikosini kutokana na majeraha ambayo yalitajwa kumuweka nje kwa wiki mbili.

Lakini kilichowastaajabisha watu wengi ni baada ya jana nyota huyo kuonekana akiitumikia klabu yake kwa dakika 18.

20:00 Ivory Coast vs Nigeria.

Makala Nyingine

More in AFCON