Klabu ya Barcelona kwa muda mrefu imekuwa ikimfuatilia kwa karibu nyota wa klabu ya Manchester United Manson Greenwood anayekipiga kwa mkopo kwenye klabu ya Getafe kwa mkopo ili kumsajili mwezi wa sita [6].
Greenwood [22] amewaambia washauri wake kuwa Barcelona ndio klabu yake ya ndoto kuichezea hivyo wafanye liwezekanalo dili hilo lifanikiwe.
“Barcelona wana hitaji kumsajili Manson Greenwood, na yeye anahitaji kwenda pale, kinachofuata ni timu hizo mbili kufikia makubaliano”.
“Manchester United inahitaji kumuuza nyota huyo na kocha amekubali Greenwood asirudi kikosini, maoni ni kuwa ni vyema kila upande ukiachana kwa amani”.
“Dili la Manchester United na Barcelona litahusisha ongezeko la pesa kutokana na mechi atakazocheza kwenye klabu na timu ya Taifa”.
“Mason bado anafikiria siku moja atalitumikia tena Taifa lake”.
“Kitu ambacho anakifanya kwasasa Mason ni kutengeneza jina Laliga na ndio maana Barcelona wamemuona”.
“Barcelona wanafikiria ndiye mchezaji atakayewapeleka kwenye hatua nyingine ya mafanikio kuanzia mashindano ya ndani na ya kimataifa”.
“Wanafikiri huu utakuwa usajili bora kwa mashabiki, na wamewatuma maafisa kumtazama zaidi ya mara sita msimu huu na majibu yamekuwa mazuri”, kiliweka wazi chanzo cha karibu cha nyota huyo.
Msimu huu nyota huyo amecheza michezo 16, amefunga magoli matatu [3] na pasi za mwisho nne [4], Valencia na Real Sociedad pia zinamfuatilia kwa karibu.
Kocha wa Getafe Jose Bordalas amesema;
“Greenwood ni mchezaji wa tofauti sana, ana kipaji kikubwa sana, lakini kwenye mpira wa sasa kipaji sio kila kitu, inahitajika juhudi kubwa kuliko kipaji”.
“Tulikuwa na imani kwasababu ya kipaji na kiwango alichonacho”.
“Kuwa na mchezaji wa kiwango hiki kwenye timu kama Getafe ni ngumu muda mwingine haiwezekani kabisa, kutokana na hali yake tulibahatika kuwa nae”.
“Tunafuraha kwasababu tunamchezaji mkubwa, ni kijana mzuri, ametosha sana na anahitaji kujifunza kidogo kihispania”.