Connect with us

AFCON

IVORY COAST YAWAFUKUZA SENEGAL AFCON 2023.

Timu ya Taifa ya Ivory Coast imetoa mshtuko mkubwa kwa wapenzi wa soka Duniani baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi timu ya Taifa ya Senegal kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penalty.

Mchezo huo ulipigwa kwenye dimba la Charles Konan Banny na kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 kwa dakika zote 120 za mchezo na baadae Ivory Coast wakaichapa Senegal kwa penalty 5-4.

Senegal walikuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu wakishinda mechi zote tatu za hatua ya makundi kabla ya kuondolewa na Ivory Coast ambayo ilipata ushindi mmoja pekee kwenye hatua ya makundi.

Alikuwa ni nyota Habibu Dialo aliyeitanguliza Senegal kwa kuifungia goli la uongozi dakika ya nne [4] ya mchezo kabla ya Frankie Kessy hajaipatia goli la kusawazisha Ivory Coast kwa mkwaju wa penalty dakika ya 86 ya mchezo.

Hadi dakika 90 za mchezo zinatamatika matokeo yalikuwa 1-1 na baadae dakika 30 zikaongezwa na matokeo yakaendelea kusali hivyo hivyo, na hatimae penalty zikaamua mshindi wa mchezo huo.

Kessie alifunga penalty ya mwisho na kuipeleka Ivory Coast hatua ya robo fainali ya michuano hii na kushuhudia mabingwa watetezi wakiyaaga mashindano haya.

Makala Nyingine

More in AFCON