
Mwenyeji wa fainali za mataifa ya Afrika timu ya Taifa ya Ivory Coast leo saa mbili [20:00] usiku kuikabili Mali katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya AFCON 2023 katika uwanja wa de la Paix uliopo mji wa Bouake.
Ivory Coast imefuzu hatua ya robo fainali bila kutarajiwa baada ya kufuzu kwa nafasi ya ‘bestlooser’ kutoka hatua ya makundi na baadae kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Senegal kwenye hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalty.
Hata hivyo Ivory Coast licha ya kufuzu hatua ya robo fainali imeshinda mchezo mmoja pekee kwenye kampeni hizi na imefunga magoli mawili pekee.
Ivory Coast imekuwa ikipata matokeo mazuri kwenye uwanja huo na wana kumbukumbu ya kihistoria kwani mwaka 2008 walishinda goli 5-0 dhidi ya Madagascar.
Mali imekuwa na mwendelezo mzuri kwenye michuano hii ikichangiwa na uimara wa golikipa wake anayekipiga kwenye klabu ya Yanga Djigui Diarra aliyeruhusu goli 2 pekee hadi hivi sasa na pia mshambuliaji wake kinara Lassine Sinayoko aliyefunga goli tatu [3] hadi hivi sasa kwenye michuano hii.
Timu ya Taifa ya Ivory Coast iliyopo chini ya kocha wa muda na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Emerse Fae imefungwa magoli sita [6] kwenye mechi tatu za mwisho, watakuwa na kazi nzito kuizuia Mali iliyofunga goli tano [5] kwenye mechi tatu [3] za mwisho.
Kaimu kocha mkuu wa kikosi cha Ivory Coast Emerse Fae amesema kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu sana kutokana na Mali kuwa na viungo wengi wazuri.
“Baada ya kufuzu dhidi ya Senegal, tuliweza kuonyesha rangi yetu halisi kitu ambacho hakikuwa rahisi kwetu kuanzia mwanzo, lakini kushinda hasa baada ya kwenda penalty inagusa sana”.
“Timu ya Mali ni nzuri, wana viungo wazuri sana na tunajua itakuwa ngumu lakini pia hata sisi ni wagumu”.
“Mimi sio mtu wa miujiza na sijawahi kufanya miujiza kivyovyote vile, lakini pia mimi ni kocha kijana ambaye nalijua hili kundi vizuri sana”.
“Nimekuwa nao kwa mwaka mmoja na nusu, baada ya mauza uza tuliyopata dhidi ya Equatorial Guinea, nilikuwa na kujiamini kwenye kikosi na niliweza kuwapa maneno ya ujasiri na ushujaa”.
“Tumeandaa timu ambayo itacheza na Mali, tumejiandaa kwa ubora, tuna ubora wetu lakini kitu mhimu tunaangalia zaidi timu yetu”.
Nyota wa kikosi cha Ivory Coast Yahia Fofana amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Mali utakuwa mgumu sana lakini hawatawadharau kwasababu wana timu nzuri.
“Tunaenda kuukabili mchezo huu tukiwa na morali ya kutosha, unaenda kuwa mchezo mgumu dhidi ya Mali, na hatutawadharau kwasababu wapo vizuri”.
Kocha mkuu wa kikosi cha Mali Eric Sekou Chelle amesema mchezo wa leo utakuwa wa hisia sana kutokana na undugu uliopo kati ya Ivory Coast na Mali.
“Tunafuraha kuwa hapa, tulipata muda wa kurejesha utimamu wa mwili na kujiandaa kwaajili ya mchezo huu”.
“Huu ni mchezo wa mtoano na utakuwa mchezo wa kuacha alama kwetu na tunatarajia makubwa kutoka kwenye huu mchezo”.
“Tunaendelea kupambana kabla ya kila mchezo hasa kwenye eneo la ulinzi na tunazidi kuimarika kila siku, washambuliaji wanafanya kazi na kitu kibuwa ni ushirikiano wa timu”.
“Mchezo huu unaenda kuwa wa hisia kubwa, unaenda kuwa mchezo dhidi ya ndugu wawili, kuna wachezaji Ivory Coast wana uhusiano kutoka Mali kwahiyo utakuwa mchezo wa kugusa hisia sana”.
Mchezaji wa kikosi cha Mali Lassine Sinayoko ameeleza kuwa mawazo yao yote yapo kuelekea mchezo wa leo.
“Tuko timamu kiakili, timu inaendelea vizuri kwaajili ya mchezo huu, mawazo yetu tumeyaelekeza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast”.
Mchezo huo utapigwa saa mbili [20:00] usiku wa leo na mshindi atafuzu kuelekea hatua ya nusu fainali ya michuano hii ya AFCON 2023.

Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 1 year agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 1 year agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 12 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 12 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 1 year agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...