Simba wamezidi kuwasogelea vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga kwa kufikisha alama 36, alama 4 nyuma ya vinara hao wenye alama 40 baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa JKT Tanzania wa Meja Jenerali Isamuhyo ikiwa ni mara ya kwanza kuutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani msimu huu.
Mchezo ulianza kwa kasi ya chini huku JKT Tanzania wakiwa na nidhamu kubwa sana kiulinzi wakishambulia kwa kutumia mipira mirefu huku silaha zao za mipira hii wakiwa Shiza Kichuya na Sixtus Sabilo.
Kama sio umahiri wa golikipa Ayoub Lakred, JKT Tanzania wangepata bao la utangulizi dakika ya 13 ya mchezo kupitia kwa Najim Magulu aliyepata nafasi akiwa peke yake na kipa baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Said Ndemla lakini alikuwa imara Lakred kuzuia mpira uliopigwa na Magulu.
Sadio Kanoute alitengenezewa nafasi nafasi nzuri ya kufunga bao na Clatous Chama lakini shuti lake halikuwa na nguvu na kuishia mikononi mwa Yakubu Selemani.
JKT Tanzania walijibu mapigo kupitia kwa David Bryson aliyejitengenezea nafasi na kuachia shuti akiwa nje kidogo ya lango la Simba lakini Ayoub Lakred alikuwa sambamba na mpira huo.
Simba walitangulia kupata bao kupitia kwa David Clatous Chama dakika ya 32 ya mchezo akipokea pasi nzuri ya usaidizi kutoka kwa Saido Ntibazonkiza na yeye kuachia shuti kali nje ya 18 ya JKT Tanzania na mpira kutinga moja kwa moja wavuni ukimshinda golikipa Yakubu Selemani.
Simba walizidi kuonyesha nia ya kuutawala mchezo wakiendelea kusukuma mashambulizi, dakika ya 44 mpira wa adhabu wa Clatous Chama kutokea upande wa kulia ulitua kichwani mwa Saido Ntibazonkiza lakini mpira ukaenda nje ya lango.
Mpaka mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0
Kipindi cha pili Walirejea kwa kasi JKT Tanzania kujaribu kutafuta bao la kusawazisha na almanusura wafanikiwe dakika ya 49 dakika ya 4 tu ya kipindi cha pili kupitia kwa Sixtus Sabilo baada ya krosi ya Shiza Kichuya kushindwa kumilikiwa vizuri na Ayoub Lakred, hata hivyo Lakred alisahihisha makosa yake kwa kuokoa shambulio hilo.
Dakika ya 55, JKT Tanzania walifanya mabadiliko ya kiufundi wakiingiza kasi mpya ya ushambuliaji kwa kumuingiza Hassan Kapalata na Aziz Kader nafasi za Sixtus Sabilo na Shiza Kichuya huku Simba wakifanya mabadiliko ya lazima Freddy Kouablan akichukua nafasi ya majeruhi Kibu Denis.
Mabadiliko ya JKT Tanzania yaliwafanya Simba waishi kwenye nyakati za mashaka huku imlazimu golikipa Ayoub Lakred kufanya kazi kadhaa za ziada.
Ismail Azizi Kader dakika ya 65 alikuwa kwenye nafasi ya karibu zaidi kuisawazishia JKT Tanzania baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Najim Magulu lakini Ayoub Lakred alimkatalia mpira wake alioupiga na kuwaweka Simba Salama.
Simba hawakuwa bora hasa dakika za mwisho ikiwalazimu kufanya mabadiliko ya wachezaji na hata kimbinu wakiamua kujilinda zaidi.
Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza, Fabrice Ngoma nafasi zao zilichukuliwa na Israel Mwenda, Luis Miquissone na Pa Omar Jobe huku JKT Tanzania wakimtambulisha Edward Songo nafasi ya Najim Magulu wakiendelea kusukuma kutafuta bao la kusawazisha.
Pa Omar Jobe alipata nafasi ya kuandika bao la 2 dakika za mwisho kabisa lakini walinzi wa JKT Tanzania walimbana na kutofanikiwa kutimiza azma yake.
Tatu Malogo alifunga mchezo huo kwa filimbi yake ya mwisho dakika zote 90 kutamatika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...