Connect with us

CAF Champions League

YANGA INA WAKATI MGUMU KUFUZU ROBO FAINALI CAF CL.

Baada ya Al ahly na CR Belouizdad kutoka suluhu ya bila kufungana inaiwafanya Al Ahly waongoze kundi kwa alama sita huku timu inayofuata ikiwa na alama tano na kuipa wakati mgumu pia Yanga wa kufuzu hatua ya robo fainali.


?? Al Ahly ____________pts6
?? CR Belouizdad______pts 5
?? Yanga SC___________pts5
?? Medeama SC________pts4

Yanga na CR Belouizdad zinalingana alama lakini utofauti wao ni magoli ya kufunga na kufungwa na kulingana na mechi zilizosalia Yanga ina wakati mgumu zaidi wa kufuzu hatua inayofuata.

Mchezo utakaoamua hatma ya Yanga ni ule dhidi ya CR Belouizdad utakaopigwa kwenye dimba la Mkapa, Jijini Dar Es Salaam, Gamond ana wakati mgumu sana hapa.

Yanga imesaliwa na michezo miwili dhidi ya CR Belouizdad ikiwa nyumbani na dhidi ya Al Ahly ikiwa ugenini, CR Belouizdad imesaliwa na mechi mbili pia dhidi ya Yanga na Medeama, yoyote atakaye changa karata zake vizuri atafuzu robo fainali.

MECHI ZIJAZO
?? Medeama SC vs Al Ahly ??
?? Yanga SC vs CR Belouizdad ??

Makala Nyingine

More in CAF Champions League