Connect with us

CAF Champions League

WAPINZANI WA YANGA, CR BELOUIZDAD KUWASILI NCHINI JUMATANO.

Klabu ya Yanga imetangaza kucheza michezo yake yote iliyopangwa kwenye ratiba bila kuomba kusogezwa mbele kwa kigezo cha michezo ya kimataifa kama ambavyo Simba ilifanya.

Ali Kamwe ameweka wazi hilo hii leo na kusema kuwa kesho watacheza mchezo wao wa ASFC dhidi ya Polisi Tanzania kama kawaida na kuwataka mashabiki kujitokeza kushuhudia dozi waliyoiandaa kwaajili ya CR Belouizdad.

“Tumezungumza na benchi la ufundi wakatuambia tucheze mechi zetu”.

“Tukiwa tunaelekea mechi ya jumamosi dhidi ya CR Belouizdad kesho pale Chamazi, tutakuwa na mchezo wa ASFC dhidi ya Polisi Tanzania”.

“Tumeona hakuna sababu ya kudeka deka, hakuna sababu ya kujificha, timu inatakiwa icheze ili kupata utimamu wa mwili [Match Fitness]”, amesema Ali Kamwe, Afisa Habari Yanga.

Ali kamwe pia ameeleza kuwa wapinzani wao klabu ya CR Belouizdad inatarajiwa kushuka nchini siku ya Jumatano asubuhi huku akitaja viingilio vya mchezo huo pia.

“Belouizdad inatarajiwa kuingia nchini siku ya Jumatano asubuhi”.

“Viingilio vya mchezo ni Elfu 30 [VIP A], Elfu 20 [VIP B] na Elfu 10 [VIP C] na Elfu 5 [Mzunguko]”, Aliongeza Kamwe.

Klabu ya Yanga imekuwa na utaratibu wa kuziita majina ya wachezaji mechi zao za kimataifa kama ambavyo pia mchezo huu walivyoupa jina la nyota wao Pacome Zouzoua raia wa Ivory coast.

“Kwenye mchezo wetu jumamosi utakuwa ni ‘PACOME DAY, kitaalamu zaidi’, ukiweza kupaka rangi kichwani, kwenye ndevu au kujipaka rangi usoni fanya hivyo”, Alimaliza Ali Kamwe.

Klabu ya Yanga na CR Belouizdad zimekutana mara moja kwenye mchezo uliomalizika kwa Yanga kupokea kichapo cha goli 3-0 ugenini na sasa ni wakati wa Yanga kulipa kisasi mbele ya CR Belouizdad.

Msimamo wa kundi hadi hivi sasa.

Al Ahly ————— Pts 6
CR Belouizdad — Pts 5
Yanga —————- Pts 5
Medeama ———- pts 4

Timu yoyote kutoka kundi hili ina uwezo wa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na mchezo huu lazima Yanga ishinde ili ijiweke kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League