Connect with us

CAF Champions League

KOCHA SIMBA AKIRI UGUMU WA MCHEZO LEO.

Klabu ya Simba ina malengo ya kuondoka na alama tatu kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Asec Mimosas utakaopigwa majira ya saa nne usiku.

Bechikah ameweka wazi kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa upande wao kutokana na faida ya wenyeji wao kuwa nyumbani lakini watapambana wapate alama tatu.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, tunahitaji kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua robo fainali, malengo yetu ni kupata alama tatu”.

Kwa upande wa golikipa wa klabu ya Simba Aishi Salum Manula ameweka wazi kuwa hawaogopi uwanja kujaa mashabiki kwani wao wanapenda kucheza kwenye uwanja uliojaa mashabiki.

“Kwa vyovyote itakavyokuwa lazima tupate matokeo, kwetu ni mechi ya mkakati na ya kupambana zaidi ili tuhakikishe tunapata matokeo kwenye mchezo huu”

“Kucheza uwanja ukiwa na mashabiki wengi sisi kama Simba huwa tunafurahia, unaposikia makelele kuna kitu kinaongezeka unahisi kweli hii ni Champions league ya Afrika”, Aishi Manula, Golikipa wa Simba.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League