Connect with us

Yanga

RAGE: KOCHA IVORY COAST ALIKOSEA KUMUACHA PACOME.

Klabu ya Yanga mwisho wa wiki iliyopita ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa Ligi ya mabingwa hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad, mchezo huo ulikuwa ukiihitaji Yanga kupata ushindi zaidi na ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0.

Matokeo hayo yaliifanya Yanga ifuzu kwenda hatua ya robo fainali huku ikiwa na mchezommoja mkononi na ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Yanga kuelekea mchezo huo waliitengeneza siku hiyo maalumu wakiita kwa jina la mchezaji wao Pacome, siku hiyo ikijulikana kama PACOME DAY, na nyota huyo alikuwa kwenye kiwango bora sana ambacho kilimfanya kila mpenda soka ausifie uwezo wake.

Uwezo wa nyota huyo ulimuibua mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage na kusema kuwa kwa uwezo aliouonyesha nyota huyo alipaswa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kilichobeba ubingwa wa Mataifa ya Afrika.

Ningekuwa na namba ya kocha wa Ivory Coast ningempigia na kumkosoa kwa kumuacha Pacome Zouzoua kwenye michuano ya AFCON 2023.

Ismail Rage Mwenyekiti wa zamani wa Simba Sc.

Pacome Zouzoua amekuwa na kiwango bora sana tangu alipojiunga na kikosi cha Yanga hadi hivi sasa kwenye michuano ya kimataifa amefunga magoli matatu [3] na kwenye Ligi amefunga magoli sita [6].

Makala Nyingine

More in Yanga