Connect with us

Makala Nyingine

MWEKEZAJI ADAI KUINUNUA KLABU MIAKA MITANO NYUMA.

Mdhamini wa klabu ya Simba na mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Mohamed Dewji ameeleza kuwa moja ya jambo ambalo anapaswa kujivunia na alitumia gharama kubwa kwenye ununuaji wake ni wa kuinunua Simba.

“Kitu cha gharama zaidi kukinunua kwangu nafikiri ni timu ya mpira inayoitwa Simba ina mashabiki million 35.”

“Nilikuwa naipenda Simba nilipokuwa kijana mdogo, niliinunua hii klabu miaka mitano iliyopita, nimeifanya hii klabu kuwa miongoni mwa timu 10 bora Afrika”.

“Ni jambo kubwa, linaleta furaha kwa watu, kwa waafrika na nina furaha sana.”

  • Mohamed Dewji

Dewji kwa muda mrefu anahesabika kama mwekezaji wa klabu hiyo lakini kwa kauli aliyoitoa inaleta kigugumizi kwa mashabiki wengi wa soka kushindwa kujua kama anaimiliki klabu hiyo au amewekeza.

Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhiidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa jumamosi hii saa [19:00] jioni katika dimba la Benjamin Mkapa.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine