Connect with us

NBC Premier League

AZAM FC YAWEKA KIKAO KIZITO KABLA YA MECHI NA YANGA.

Viongozi wa Azam FC walikutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi ikiwa ni siku chache kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga, baada ya klabu hiyo kuchapisha picha za kikao hicho kwenye mitandao yake ya kijamii, wadau wamehusisha kikao hicho kuwa ni mipango na mikakati kuelekea mchezo wao dhidi ya Wananchi.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC Zaka Zakazi amesema kikao hicho ni cha kawaida na kimefanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mwaka huu.

“Hakuna kitu cha tofauti, kuna namna kwamba hii mechi [Yanga vs Azam FC] ina treatment ya kipekee ndio maana hata kikao hiki hakihusu hii mechi! Kina husu sehemu ya Ligi iliyokuwa ndani ya mwaka 2024 kwa sababu viongozi hawakupata muda wa pamoja kukutana na wachezaji kama vile.”

“Kwa hiyo hiki kikao kinahusu mechi zilizopita ndani ya mwaka 2024 na mechi zilizobakia msimu huu. Kwa hiyo hii mechi sio maalum kiasi hicho hadi kuwa na zawadi za pekeake, hapana. Ni mechi muhimu, ni mechi ambayo itatufungulia msimu wetu kwa sehemu iliyobakia lakini mioyo na akili za wachezaji ni muhimu kuliko hela zinazokuwa mezani kwao.”

“Kama unataka kumnywesha maji mbuzi, utampeleka kisimani lakini kama hataamua kufungua mdomo hawezi kunywa hayo maji. Kwa hiyo ni wachezaji wenyewe waamue kucheza, wakiamua kucheza na kupata matokeo mazuri hayo mengine yatakuja tu.”

“Hadi sasa kilakitu kipo kama kawaida ambavyo wenyewe wanajua inavyokuwa.”- Zaka za kazi, Afisa habari Azam FC.

Mchezo wa Azam na Yanga utapigwa kesho jumapili saa mbili [20:30] usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League