Connect with us

Chelsea

NYOTA WA ZAMANI WA CHELSEA LOIC REMY ATUNDIKA DALUGA.

Remy ametangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 36, baada ya mkataba wake na Brest kutamatika.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Loic Remy ametangaza kustaafu kucheza soka la ushindani akiwa ana umri wa miaka 36.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa ametangaza kustaafu kucheza soka la kulipwa mara baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya klabu ya Brest inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa.

Loic alicheza michezo 47 akiwa na Chelsea na kufunga magoli 12 huku akitoa pasi za usaidizi wa magoli 3, ameshinda kombe Ligi kuu (EPL) moja (1) na kombe la Ligi (FA) moja (1).

Makala Nyingine

More in Chelsea