Connect with us

AFCON

TANZANIA YAPANGWA KUNDI F AFCON 2023, IVORY COAST.

Tanzania itakutana na timu ya Taifa ya Morocco, Zambia na DR Congo kwenye kundi F.

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF usiku wa leo limeendesha droo ya upangaji wa makundi Jijini Abdjan, Ivory Coast kwa timu zilizofuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2023) zilizopangwa kupigwa January 2024. Tanzania ni miongoni mwa nchi 24 zilizofuzu kushiriki mashindano haya yatakayofanyika nchini Ivory Coast.

Timu ya Taifa ya Tanzania imepangwa kundi F, ikiwa sambamba na mataifa ya Zambia, DR Congo na Morocco. Hizi ni makala za tatu za AFCON kwa Tanzania kushiriki baada ya kufanya hivyo mwaka 1980, 2019 na 2023. Michezo yote ya kundi F itapigwa katika mji wa San Pedro, mji uliopo kusini mashariki mwa Ivory Coast.

Kundi A. Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea Bissau

Kundi B. Misri, Ghana, Cape Verde, Msumbiji.

Kundi C. Senegal, Cameroon, Guinea na Gambia.

Kundi D. Algeria, Burkina Faso, Mauritania, na Angola.

Kundi E. Tunisia, Mali, Afrika Kusini na Namibia.

Hafla hizo zilihudhuliwa na watu mbalimbali akiwemo Rais wa CAF Patrice Motsepe, Marais wa mashirikisho mbalimbali Barani Afrika wanasoka wa zamani kama Yaya Toure, Didie Drogba, Achraf Hakimi, Obi Mikel na wengine wengi.

Katika hafla hizo za upangaji makundi Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika Patrice Motsepe alisema kuwa anaamini kwa namna ambavyo soka la Afrika linapiga hatua kwa miaka ijayo Afrika itatoa Bingwa wa kombe la Dunia huku akitoa mfano wa timu ya Taifa ya Morocco ambayo ilifika nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Duniani na kusema kuwa kwa wakati mwingine hawataishia hapo watafika fainali na watabeba ubingwa.

kwa upande mwingine Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika Patrice Motsepe amesema kuwa ili kupata wanasoka bora kama walivyokuwa kina Didier Drogba, Yaya Toure au ilivo kwa Mohamed Salah na Sadio Mane ni lazima kuwekeza kwenye soka huko mashuleni, na ndio maana kwasasa shirikisho la soka Afrika limeanzisha mashindano rasmi ya ngazi ya shule.

Makala Nyingine

More in AFCON