Wakala wa kocha mkuu wa kikosi cha Liverpool Jurgen Klopp, Kosicke amethibitisha kuwa mteja wake hatajiunga na timu ya Taifa ya Ujerumani kama ilivyoripotiwa hapo awali ili kuchukua mikoba ya Hans Flick aliyetimuliwa kikosini hapo kutokana na timu hiyo kupata matokeo yasiyoridhisha.
Kosicke amesema mteja wake ana mkataba wa muda mrefu na klabu ya Liverpool hivyo kwasasa nguvu zake ziko kwenye kuijenga timu hiyo na kuipa ushindi.
Hans Flick aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani.
Hans Flick alijiunga na kikosi hicho mwaka 2021 akitokea katika klabu ya Bayern Munich na aliondoshwa kufuatia matokeo mabaya aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Japan alipokubali kipigo cha goli 4-1.