Kiungo mshambuliaji wa klabu ya soka ya Manchester United ya UIngereza, Jadon Sancho ameamua kuufunga ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram hii leo.
Kutokana na hali yake ya sintofahamu ndani ya United baina yake na Kocha wke Erik Ten Hag, Sancho ameona anahitaji kujiweka kando na mitandao ya kijamii ili aweze kupambana na hali yake ya sasa. Erik alishasema kuwa hali yake ndani ya United iko chini ya mikono yake mwenyewe.
Kwa hali ilivyo, ni aidha Sancho aombe radhi aendelee kuwepo kwenye timu au auzwe dirisha dogo Januari.