Klabu ya Yanga kupitia Afisa Habari wake Ali Kamwe leo imetangaza mchezo wao wa maruadiano dhidi ya El Merreikh Jumamosi hii Septemba 30 wameupa jina maalumu “Ki Day” wakimaanisha ni siku ya mchezaji wao Aziz Ki.
Ali Kamwe amesema kuwa siku hiyo wanaenda kufungua mlango wa kuingia hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika ambao wameshindwa kuufungua kwa muda mrefu,na ndio maana wameuita “Ki Day”
Yanga walishinda mchezo wa kwanza ugenini kwa goli 2-0 na kwenye mchezo wa marudiano wanahitaji sare yoyote tu kufuzu hatua ya makundi.