Azam FC

AZAM HAIWEZI KUBEBA UBINGWA ~ KOCHA MINGANGE.

Kocha wa zamani wa timu ya vijana ya Azam Meja Abdul Mingange amesema Azam haiwezi kuwa bingwa kwasababu viongozi wanaosimamia mpira wapo Simba na Yanga.

Published on

Kwasababu viongozi wanaosimamia mpira wapo Simba na Yanga.
Kiungo wa Azam FC Feisal Salum akimtoka kiungo wa klabu ya Yanga kwenye michuano ya ngao ya Jamii, Tanga.

Mashabiki wa soka nchini wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu klabu ya Azam kutoonyesha ushindani wa kutosha kwenye Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na hata katika michuano ya Kimataifa licha ya kuwa na miundombinu rafiki ambayo ingeifanya klabu hiyo kuwa bora, kuhusu hili Dauda Sports ikafanya mahojiano na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Vijana ya Azam fc Abdul Mingange.

Mingange amesema kuna sababu nyingi sana zinazoifanya Azam fc isifanye vizuri katika mashindano yote licha ya kuwa na miundombinu rafiki ambayo ingeifanya timu hiyo iwe na ushindani kuanzia Ligi kuu kandanda Tanzania Bara hadi michuano ya kimataifa.

Miongoni mwa sababu alizozitaja ni pamoja na viongozi wengi wanaosimamia mpira wapo kwenye makundi ya Simba na Yanga kitu ambacho wakati mwingine kina wanyima haki wanayostahili.

Yanga na Simba wakiwa kwenye ubora wao Azam hawezi kupenya kwasababu wanaosimamia mpira,wapenzi na watu wote wako katika haya makundi mawili kwahiyo wanabanwa katika sehemu hiyo.

Abdul Mingane kocha wa zamani wa timu ya vijana ya Azam fc kuhusu kutokufanya vizuri Ligi kuu.

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli katika mchezo wa Ligi

Kuhusu kutokufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa sehemu ambayo hawakutani na klabu za Simba na Yanga Abdul Mingange amesema tatizo lipo kwenye uongozi wa klabu hiyo hasa kubadilisha walimu mara kwa mara, Azam hawana uvumilivu.

Azam walikuwa na Cioaba mwalimu mzuri sana mimi nimekaa nae, hakuna timu isiyofungwa wao sio wavumilivu wa kukaa na walimu na hilo linachangia sana kutokupata mafanikio, Simba wamefanya uvumilivu kwa Robertinho ina walipa na Yanga kwa Nabi, mwalimu akikaa na timu muda mrefu anajua mapungufu na anayarekebisha.

Mingange pia amesema suala la viongozi wa klabu kuwapangia makocha kikosi lipo kwa sana na ndilo linalorudisha nyuma soka la klabu ya Azam.

https://daudasports.co.tz/wp-content/uploads/2023/10/MEJA-ABDUL-MINGANGE.mp3
Meja Abdul Mingange akieleza sababu za Azam kutokufanya vizuri

Popular Posts

Exit mobile version